Aliyepanga Kumuua #TunduLissu ni Huyu Anayejiita @UsalamaWaTaifa , Alihusika Pia Kwa Ulimboka Na Kubenea

Kwa mnaofuatilia maandiko yangu mbalimbali mtandaoni, mnafahamu fika kuwa sijawahi “kuwalisha matango pori.”

Na katika mwendelezo huo wa kutowalisha matango pori, kwa hakika ya asilimia 100 ninaufahamisha umma kuhusu mtu aliyehusika kwa asilimia 100 kupanga na kutekeleza jaribio la kumuua Tundu Lissu. Mtu huyu ni mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa, akiwa mwandamizi katika ngazi ya mkoa, na yupo katika mtandao wa kijamii wa Twitter akitumia jina @UsalamaWaTaifa

Taarifa hii nimeithibitisha kupitia vyanzo tofauti vitano. Na kimsingi, taarifa hiyo ilipatikana bila kukusudia. Binafsi nimekuwa nikiifuatilia akaunti hii kitambo kwa sababu wakati fulani huko nyuma iliwahi kuweka mfululizo wa tweets kunihusu mie na baadhi ya wanaharakati wa mtandaoni. Awali akaunti hii ilikuwa inahusiana na nyingine iliyotumia jina @AgentX_Tz

Ni katika kufuatilia huko ndipo jana nikafanikiwa kuelezwa utambulisho halisi wa mhusika. Lakini kilichonigusa zaidi — na ndicho kilichonisukuma kuandika makala hii — ni taarifa kwamba mtu huyu ndiye mhusika mkuu wa jaribio lililofeli la kutaka kumuuwa Tundu Lissu.

Taarifa zinazeleza kuwa shambulio hilo lilifanywa na “kitengo nje ya kitengo”, kile kinachofahamika kama “kikosi maalumu” kilichokuwa chini ya usimamizi wa Bashite. Kikosi hicho kilikuwa na mchanganyiko wa maafisa wa “Idara halisi” ya Usalama wa Taifa (hii tunayoifahamu), JWTZ na Polisi. Kadhalika, kikosi hicho kilikuwa kikipata sapoti kutoka maafisa usalama wa taifa wa nchi moja jirani.

Sasa huyu bwana licha ya kueleza kwenye akaunti yake kuwa hana uhusiano na “kitengo” lakini ukweli ni kwamba ni mwandamizi katika mkoa fulani anaouongoza. Kadhalika, takriban miaka minne iliyopita, mtu huyu aliongoza operesheni mbili zinazoshabihiana na hiyo aliyoshiriki dhidi ya Lissu: kutekwa na kuteswa na Ulimboka na tukio la kumwagiwa tindikali mwandishi Saed Kubenea.

Na kama ilivyotokea kwa Ulimboka na Kubenea, wahusika katika tukio la kujaribu kumuua Lissu wanaonekana kupewa kinga licha ya unyama walioufanya.

Nihitimishe makala hii kwa kutoa tahadhari ifuatayo: jisikie huru kutoamini taarifa hii, lakini kama una nafasi na dhamira ya dhati ya kufahamu waliomtendea unyama Lissu, basi angalau jihangaishe kuthibitha iwapo nilichoandika ni kweli au ni “matango pori.”

Kwa ndugu zangu wa Chadema, ushauri wangu kwenu ni huu: mtu wenu ni huyu @UsalamaWaTaifa . Mkijibidiisha kidogo tu mtafahamu jina lake halisi japo mkiunganisha dots na tukio la Ulimboka na Kubenea hamuwezi kushindwa kufahamu.

Kwa ninyi mnaofuata “ubuyu wa ushushushu” kwenye akaunti hiyo, nachoweza kuwashauri ni kuwa makini. Simshauri mtu afanye ku-unfollow akaunti hiyo lakini mjue tu “mnacheza na moto.”