Burhani M Mustapha
Nov 2 · 2 min read

WEWE NI WA THAMANI

Ni sentensi moja tu inayoweza kukupa hamasa ya kusonga mbele, hamasa ya kupambana zaidi huku ukitambua kwamba “Hauna Muda” wa kutosha hapa duniani. Sentensi hiyo ni hii “KUNA SIKU UTAONDOKA HAPA DUNIANI.”

Umezaliwa mara moja tu, hakuna wakati mwingine tena utakapozaliwa na kurudi upya duniani; na hii ndio fursa pekee ya kutengeneza Furaha katika maisha yako (Kwa kitimiza malengo na kufikia ndoto zako). Badala ya kukaa na kulalamika kwa kushindwa kufikia malengo yako (kushindwa kutimiza wajibu wako ipasavyo), Fanya kitu ili kukabiliana na hali hiyo (Wajibika ipasavyo!).

👉Maisha unayotamani kuishi. “Bila kujali UMRI wako, bado una nafasi ya kutengeneza Furaha unayoitaka katika maisha yako.”

Kama upo katika umri wa miaka 20s, kwa asilimia kubwa na uhalisia wake, wewe ni kijana; una nguvu na nafasi kubwa ya kuchagua aina ya maisha unayotaka kuishi leo na huko baadae. Huu ni wakati wa kutumia kila fursa muhimu inayokuja mbele yako. Tengeneza Network ya kutosha na watu, weka malengo, fanyia kazi ndoto zako na hakikisha unatengeneza mahusiano bora na yenye manufaa kwako.

Kama umevuka umri wa ujana na upo katika miaka ya 50, 60, 70 na kuendelea, badala ya kusubiri ustaafu na kurudi kukaa nyumbani, unaweza ukawa ndio muda mzuri wa kuwekeza katika mambo unayopenda kufanya au kuwekeza zaidi kwa vijana.

👉Acha kutafuta sababu za kughairisha kutimiza wajibu/malengo yako.

Kuna hii tabia ya watu kughairisha kutimiza wajibu wao/malengo waliyojiwekea kwa kujipa katumaini kwamba; “Watafanya wakati mwingine”. Asilimia kubwa ya watu wanaishi maisha yao wakidhani kwamba, wataendelea kuwepo milele hapa duniani. .

Sumu kubwa (Tatizo) tunayokumbana nayo sisi binadamu pale tunaposhindwa kutimiza wajibu/malengo yetu ipasavyo ni “MAJUTO”. Hivyo basi, acha kutafuta sababu za kughairisha kutimiza wajibu/malengo yako, anza kuwajibika na kutengeneza Furaha yako leo (Kwa kutimiza malengo na kufikia ndoto zako ambazo kwa pamoja huzaa mafanikio).

Nakutakia Safari njema katika kutafuta mafanikio. Mungu aendelee kukubariki na kukuongoza vyema katika safari hiyo.

    Burhani M Mustapha

    Written by

    Director Tuvuke Wote Organisation (T.W.O)