Nakupenda
Ngomeni son.
Sio tu kukupenda, nakuheshimu pia
Upendo ulio nipa, naahidi kukulinda
Nitapambana kukutetea, ahadi nakupa
Sito jaribu kukuacha, mbali ukaenda.
Nakupenda sana, sahau kuwa nitakutenda
Naamini wewe nimeletewa ,tuwe wote katika dunia
Tamaa yangu unaijua, nikuwa nawe daima
Naamini tuliyo panga, karibu twayafikia
Nakumbuka, ulivyo pambana
Kunilinda na kunitetea, na kunipendezesha
Niwe mbali hukutaka, Huzuni moyo ulijaa
mazoezini hukutaka, kuchelewa kurudi hukutaka
Uliyo fanya wasitaili tuzo, siwezi hadithia uzuri wako
Mengi yenye manufaa unayo, umenijenga kwa upendo wako
Matamu mapenzi yako , sihishiwi hamu kwako
Nakupenda peke yako, leo hata kesho.
Tamaa yako, ilikuwa niwewako
Nami sasa niwako, leo hata kesho
Thamani yako, ni yakwako peke yako
Ni upendo wako , ndiyo furaha na amani ya moyo
Uliumia nilipo kukosea, hukusita kuniambia
Ulinikanya na kunirekebisha, nilipo hama njia
Wivu na hisia zako zimejaa, ni kwajili ya penzi ulilo nipa
Sito kuacha ahadi nakupa , nitakuoa kipenzi hiyo chukua.