#SimuliziHai
Siku moja, Ukweli na Uongo, walikutana, usishangae! Maisha ni mikutano isiyo na kikomo.
Uongo, akamkaribia Ukweli na kumsalimia, akisema:
-“good morning, komredi Ukweli!”
Ile kusikia salamu, bila unafiki, Ukweli akaamua kujiridhisha kama kweli ni asubuhi njema. Alitazama juu akaona jua limechomoza na hakuna mawingu ya mvua, ndege wa porini walikuwa wanaimba, watu walikuwa huru kuja na kwenda. Akajiridhisha kuwa kila kitu ni sawa, hakuna udhalilishaji.
Baada ya uhakiki na uthibiti kwamba kweli siku ni shwari, Ukweli alijibu:
-“Nzuri, best Uongo”!
Leo jua ni kali sana, si ndio!- Uongo aliuliza
Ni ukweli uchi, jua liliwaka haswa. Kuona na kujihakikisha kuwa Uongo alikuwa muwazi. From there, Ukweli alianza taratibu kushusha mwavuli na kuanza kurelax. Kwa misingi ipi, Ukweli angeendelea kukosa amani, wakati Uongo alionekana kuongoka. Kuongoka sio mchezo, ni rahisi kubadilika na kubadilisha wengine.
Joto lilipozidi kuchoma, Uongo, kwa tabasamu la kisiasa akamwalika rafiki yake Ukweli waingie mtoni kuogelea!
Kwa madaha bila haba, Uongo akatoa nguo na kujirusha mtoni, huku akikazia mwaliko.
-“Njoo shosti, maji ni mazuri, utapenda mwenyewe. Uongo alipiga debe kama kama zile propaganda za Televisheni nyingi. Hapa nakumbuka somo la mchungaji wangu kwamba; “Kujustify mara kwa mara nafasi na kazi zako sio dalili nzuri”. Turudi kwenye saga letu….
Mwaliko ulimtekenya kweli kweli, basi, Ukweli akavua nguo, akajirusha mtoni pia na kuanza kuogelea. Aliogelea kwa mbwembwe zote, huku Uongo akimsoma na kumchora.
Ile Ukweli anapiga mbizi za kina, ghafla, Uongo akatoka nje na kwenda kuvaa nguo za Ukweli na kuondoka zake kwenda mitaani…..
Ukweli akashtuka kutomwona Uongo, ile kutoka kwenye maji hakuona nguo zake, alijisikia vibaya na kuwaza kuhusu muonekano wake. Nguo pekee zilizokuwepo ni za Uongo, lakini Ukweli alikataa kata kujisitiri zile nguo.
Akijiamini kuwa hana hatia na ni mtu msafi, hana haja ya kuona aibu, alitoka pale mahali akiwa uchi wa nchi..Aliamua kusimamia misingi na sio watu. Na pia aliamua kuwa yeye mwenyewe!
Tokea siku hiyo mpaka leo unaposoma hii #SimuliziHai imekuwa rahisi katika macho na maskio ya watu kuamini na kumpokea Uongo aliyevaa nguo za kuiba za Ukweli, kuliko kuamini Ukweli anayetembea uchi nchini.
HOMEWORK…Husianisha kati ya hii simulizi na mwenendo wa mambo katika jamii yetu ya kitanzania!
Byeee….Much love!
