Ripoti: Urithi wa Jamii ya Kidijitali na Ufikiaji Wazi

Bettina Fabos
Creative Commons: We Like to Share
7 min readDec 8, 2022

--

By Mariana Ziku and Bettina Fabos

Additional contributors (in alphabetical order): Alhassan Mohammed Awal, Marie-Claire Dangerfield, Maria Drabczyk, Revekka Kefalea, Jacob Moe, Ngozi Osuchukwu, María R. Osuna Alarcón.

TRANSLATION by Liz Oyange — Ngando

Utangulizi

Ripoti hii ya lugha ya kimataifa inaeleza utafiti uliofanywa na kikundi kazi cha urithi wa jamii wa kidijitali (Digital Community Heritage Working Group), katika muktadha wa ufikiaji wazi na mageuzi ya kidijitali yanayojumuisha, inayoangazia matokeo muhimu matatu:

i. Urithi unaohusiana na jamii huleta mwamko wa juu zaidi kwa kutambua kwa uwajibikaji jamii chanzo linapokuja suala la ufikiaji na utumiaji (Vézina na Muscat, 2021).

ii. Uchapishaji urithi za jamii katika ufikiaji wazi kunaweza kusawazisha mapengo ya uwakilishi katika nyanja ya umma ya jamii zisizoripotiwa na zilizotengwa (Fraser,2021).

iii. Mipango ya urithi wa jamii inaweza kujenga uwezo katika kiwango ya jamii, kuhakikisha matumizi ya zana, sera na teknolojia kwa manufaa bora ya jamii (Vézina na Nicholas, 2014).

Kufafanua Jamii

Nini ufahamu wetu wa kisasa wa jamii?Jamii ni dhana ya ugiligili, pana na yenye sura nyingi, iliyegandishwa na i. hisia ya utambulisho, ii. Hisia ya mali na, iii. mahusiano kati ya wanajamii (Dos Santos, 2012). Mkataba wa UNESCO kwa ajili ya kulinda urithi wa utamaduni usioshikika (2003), ambayo huweka mbele jamii katika muktadha wa urithi, haibainishi “jamii” kuruhusu uhuru juu ya ufafanuzi wake. Jamii zinaweza kujiamulia, kwa kutambua uwakilishi wao katika kiwango cha chini, au kutojitambulisha (jamii za kihistoria). Katika mipangilio ya kidijitali, jamii zinaweza kuwezeshwa kwa hali zaidi kwa njia “zisizo sugu”, kupitia mchango wa mtumiaji, mtandao wa kompyuta au binadamu kwa mwingiliano wa kompyuta. Bila shaka, jumuia zinaweza kuonyesha mambo yanayoingiliana na mtandao changamano wa mahusiano ambayo mara nyingi hayatambuliki kwa urahisi (Pérez López, 2014).

Mbinu

Utafiti wetu ulilenga mipango ya mtandaoni ambapo wanajamii na watumiaji nasibu huchangia sababu inayohusiana na urithi wa jamii. Tuliunda uainishaji wa aina tatu ili kupanga na kutathmini umuhimu wa mipango yote kwa mada yetu: inayoendeshwa na jamii, inayochochewa na jamii, na inayoelekezwa kwa jamii. Tulitoa uchunguzi wa umma wa lugha nyingi ili kukusanya kesi za kimataifa za urithi wa jamii ya kidijitali, pamoja na utafiti wa eneo-kazi uliofanywa na washiriki wa kikundi kazi.

Pia tuliunda uainishaji wa kategoria 10 ili kupanga aina mbalimbali za mipango ya urithi wa jamii ya kidijitali. 1. Sayansi ya raia / kutafuta umati 2. Sayansi ya jamii/ utafiti shirikishi wa jamii 3. Ushirikiano wa umati wa umma 4. Folksonomia au utambulisho wa kidijitali 5. Utunzaji pamoja 6. Sanaa ya kijamii / sanaa inayohusika ya kijamii 7. Utawala shirikishi wa data 8. Shughuli za kidijitali/harakati 9. Uhifadhi wa kumbukumbu za jamii 10. Mifano mingine ya urithi (jamii). Mipango inaweza kuangukia katika kategoria zaidi ya moja.

Tulipata kategoria mbili kuu za aina za jamii zenye kategoria ndogo tatu (3) kila moja:

i. Nguvu ya mahali (inayofungamana na eneo, na kuainishwa zaidi katika jiji, eneo na nchi)

ii. Nguvu ya kawaida (inayofungamana na hali ya kawaida, na kuainishwa zaidi katika utamaduni, maslahi na utendaji)

“Jamii nyingi” ziliongezwa kwa ajili ya mipango inayohudumia zaidi ya aina moja ya jamii.

Uwazi ndio kitovu cha utafiti wetu. Tulijumuisha aina tatu kuu:

i. kuruhusu mchango wa mtumiaji

ii. matumizi ya leseni wazi/ uwazi wa kutumia tena ubunifu

iii. ujumuishaji wa programu ya chanzo-wazi au zana.

Tuliweka mfumo rahisi wa kuweka alama ili kutathmini kiwango cha uwazi. Kwa mchango wa mtumiaji, tuliainisha aina tatu: i. kuruhusu michango ya umma (kuweka alama, kunakili, na kadhalika) ii. kuruhusu upakiaji wa umma (uwezo wa kupakia vizalia vya asili na rasilimali) iii. kuruhusu ushirikishwaji wa ushirikiano wa umma, ambao hutoa wakala wa juu zaidi na uhuru, kulingana na kiwango cha ushiriki (Haklay, 2011; Arnstein, 1969). Kwa matumizi ya leseni zilizo wazi, tulihoji ikiwa mpango huo unatumia leseni zilizo wazi kufuatia leseni za kufuata zilizopendekezwa na OKF, ikiwa imefungwa au imefunguliwa kwa matumizi ya ubunifu na, ikiwa imefunguliwa, ikiwa inaruhusu matumizi ya huria au kidogo (kuweka vikwazo kama vile matumizi ya kielimu pekee). Mwisho, tulitambua kama mipango inatumia, kuendeleza au zote mbili, programu huria au zana nyinginezo, ikijumuisha hasa kusimama pekee, programu rahisi kwa mtumiaju ambayo hutoa suluhu zilizounganishwa.

Uchambuzi

Tulikusanya data na kuzifanya ziweze kusomeka kwa machine, tulitayarisha maswali ya utafiti, na kufanya uchambuzi wa data, baadaye kuchunguza data zinazotoa taswira. Lahajedwali ya ufikiaji wazi iliyo na sifa za ziada inaweza kupatikana hapa. Tuliamua kuchambua mipango ishirini na saba (27) yafuatayo:

1 Patrimonio Mapuche de Pukon

2 Budapest 100

3 Wikimedia Nigeria

4. Reporting wildlife crime

5 Vault of Industrial Archives

6 Enterreno

7 NotreHistoire

8 Open Siddur

9 Fortepan.us

10 Fortepan.hu

11 History Harvest

12 Rotterdam Dig It Up

13 Topotheque

14 Art Pluriverse

15 Archipelago Network

16 Historypin

17 Undesign the Redline @ Barnard

18 Ajapaik

19 Ibali Digital Collections

20 MOMU Pattern-a-thon

21 Basjkieren

22 Dansk Kulturarv

23 Picturing Michigan’s Past

24 Sucho

25 Weave

26 Dokuforte

27 Queering the map

Mchoro 1: Mipango 27 ya kimataifa ya urithi wa jamii ya kidijitali iliyochaguliwa

a. Taswira za data

Mchoro 2a: Kategoria za mipango 27 ya urithi wa jamii ya kidijitali i. Kulingana na aina yao ya urithi wa jamii ya kidijitali na ii. kulingana na uhusiano wao na GLAM.
Mchoro 2b: Seti mbili za taswira i. Mtazamo wa kuunganisha kategoria za ‘’uhusiano na GLAM’’ na “aina ya urithi wa jamii ya kidijitali”. ii. Mtazamo wa pamoja wa uwanja “uhusiano na GLAM” na “aina ya mpango”.
Mchoro 3: Mwonekano wa chati ya miraba ya idadi ya mipango iliyofunguliwa kwa matumizi ya ubunifu (alama ya kijani) katika kila aina ya urithi wa jamii ya kidijitali.
Mchoro 4: Ratiba ya idadi ya mipango (mhimili wima) iliyopangwa kwa mwaka ambao kila mpango ulianza (mhimili mlalo). Alama nyekundu huwakilisha hatua ambazo hazifanyiki tena na kijani huashiria zile zinazoendelea.
Mchoro 5: Mtazamo wa ramani ya aina za jamii.
Mchoro 6: Mtazamo wa ramani wa idadi ya mipango na usambazaji wao kwenye ramani ya kijiografia.
Mchoro 7. Mwonekano wa kesi-kwa-kesi wa taipologia ya kategoria kumi (10). Kila mpango unaweza kujumuisha zaidi ya aina moja.
Mchoro 8: Mtazamo uliojumlishwa wa taipolojia ya kategoria kumi (10) na idadi ya mipango katika kila kategoria.
Mchoro 9: Mwonekano wa kesi-kwa-kesi ukichanganya uainishaji ya kategoria kumi na “kuruhusu mchango wa mtumiaji”. Juhudi nyingi katika sayansi ya raia/ukusanyaji wa watu, folksonomia au ngano za watu na uratibu wa pamoja huruhusu mchango wa mtumiaji.
Mchoro 10: mwonekano wa kesi-kwa-kesi unaochanganya kategoria za “kuanzia mwaka” na alama zao za uwazi kwa ujumla. Baa za bluu na ndefu zinaonyesha uwazi wa juu.
Mchoro 11: Orodha iliyo na mipango iliyo wazi kwa utumiaji wa ubunifu tena, bluu nzito huonyesha matumizi yaliyo wazi zaidi kwa ubunifu na bluu hafifu isiyo wazi zaidi. Nyingi ya mipango iliyo wazi zaidi kwa matumizi ya ubunifu inachochewa na jamii.
Mchoro 12: Mwonekano wa kesi-kwa-kesi unaotathmini wigo wa jumla wa uwazi wa mipango (kujumlisha nyanja za mchango wa mtumiaji, leseni huria / utumiaji upya wa ubunifu na programu huria), iliyowasilishwa kwa mpangilio kutoka kwa jumla iliyo wazi zaidi (juu) hadi ndogo zaidi (chini), kuhusiana na uainishaji ya kategoria kumi.

Maarifa

Ushiriki wa jamii kupitia mahali na mambo ya kawaida

Tumepata mandhari mahiri ya mipango ya urithi wa jamii ya kidijitali duniani kote (Mchoro 6), zinazoonyesha ushirikishwaji wa kina wa umma. Kati ya mipango ishirini na saba (27), kumi na tano (15) imeelekezwa kwa mahali, ikihudumia nchi moja, eneo au kusoma historia ya eneo la kitongoji. Majukwaa kama Topotheque ama Fortepan.us, yawapa jamii miundombinu ya kujipanga katika ngazi ya mkoa, jiji au hata kijiji. Tovuti kama Historypin na Reporting Wildlife Crime, yana ruhusu wanajamii kushiriki historia ndogo ndogo katika kiwango cha ndani kabisa (kona ya barabara, msitu).

Pia tulibainisha mipango tisa (9) inayofungamana na mambo ya kawaida, mara nyingi kukiuka mipaka na kuunga mkono hatua za kuvuka mipaka kuhusu mada mbalimbali za kitamaduni kama vile LGBTQ2IA+, urithi wa asili na wa nchi za Balkani. Haishangazi, tulipata mwingiliano wa asili kati ya jamii za kawaida na mahali.

Wakala wa kukuza jamii: kufanya kazi na, kati na nje ya GLAMs

Wanajamii wanajenga miradi, wanajiunga na majukwaa na kufanya kazi kuanzia chini kwenda juu, shughuli za ubunifu pamoja, kupakia vizalia vyao vya kitamaduni, kuongeza lebo na data nyingine ya meta kulingana na historia yao ya eneo na maarifa ya pamoja ya jamii. Mipango isiyo ya GLAM, ambayo ndiyo kesi nyingi tulizochagua (12), inawakilisha jamii mbalimbali na zisizoripotiwa katika njia za ubunifu na maadili. Mashirika yasiyo ya GLAM ndio msingi wa mipango yote inayoendeshwa na jamii katika utafiti wetu (5), inayofanya kazi kama vitoleo vya wakala wa jamii kwa ujumla, ikichukua jukumu muhimu katika kuongeza uwezo na ujuzi ndani ya jamii.

Mipango yetu mingi iliyochaguliwa ya urithi wa jamii ya kidijitali (10) iko chini ya kategoria ya kati, ambayo imeibuka katika nafasi ndogo kati ya taasisi za GLAM na miduara ya jamii na inaweza kutambuliwa kama majukwaa ya ushirika (Campbell na Fabos,2021), [Mchoro 2a]. Wanaonekana kuongoza katika uvumbuzi wazi na mara nyingi hufungamanishwa na vuguvugu la wazi, wakicheza jukumu muhimu katika kusukuma nyanja ya urithi wa kidijitali kufikiria upya uzoefu wa mtumiaji na matumizi.

Kuhamasisha Uwazi katika Urithi wa Jamii ya Kidijitali

Juhudi nyingi zilizo wazi zaidi kwa matumizi ya ubunifu pia huchochewa na jamii [Mchoro 11], na huwa na mwelekeo kuhusu sayansi ya raia/utafutaji wa watu, folkosonomia, utunzaji wa pamoja na kuhifadhi kumbukumbu za jamii [Mchoro 12]. Mipango yote ambayo ina alama za juu katika kufikia uwazi imeanza mapema kwa wakati (2009,2010,2011,2015), ilhali mipango ambayo imeanza hivi majuzi zaidi (2019–2022) haijatekelezwa kwa upana katika suala la uwazi [Mchoro 10]. Hii inaweza kumaanisha kuwa uwazi unapungua au kwamba miundo thabiti ya kidijitali iliyo wazi inahitaji muda na juhudi. Kuongezeka kwa programu huria katika miaka ya hivi majuzi kunatia moyo na kunaweza kutegemea manufaa yake katika kuchanganya matengenezo ya gharama ya chini na usimbaji shirikishi/ utatuzi wa matatizo. Hata hivyo, baadhi ya mipango muhimu inakubali mbinu iliyofungwa zaidi, ikiwezekana ikihusisha na hali ya sasa ya uwazi ambayo inaweza kudhoofisha jamii fulani au ukosefu wa ufahamu (Khan,2020). Suluhu za ziada zinaweza kuhitajika ili kuimarisha usalama na kutegemewa kwa jamii ndani ya mipangilio ya kidijitali (k.m.Local Contexts).

Mipango ya urithi wa jamii ya kidijitali inaonyesha miundo mingi ya ubunifu, endelevu na inayowajibika ya uwazi, kupitia ushirikiano kati ya jamii na umma na mipango isiyo ya GLAM, “katikati” ya majukwaa ya ushirikiano na GLAMS, ambayo ni nguvu zinazoendesha katika eneo hili la kisasa. Makubaliano yetu ya kikundi kazi ni kuhimiza njia zaidi za ufikiaji wazi na ushirikiano. Hizi zinaweza kuja kwa njia ya kujumuisha taarifa za wazi za kauli za sera na njia rahisi za kufikia programu huria. Kuunganishwa na jamii za vuguvugu huria kunaweza kukua, kutafsiri maudhui ya CC katika lugha zinazojumuisha zaidi na kuunda zana za ufikivu wazi za urithi wa jamii ambazo hujengwa juu ya mazoea mazuri, kuongeza ushirikiano kati ya jamii na kuimarisha uhuru wao, wakala na uwazi.

Bonyeza HAPA kuona ripoti kamili.

--

--

Bettina Fabos
Creative Commons: We Like to Share

Director of Fortepan.us photo history platform project; Professor of Interactive Digital Studies at the University of Northern Iowa