JE, SAUTI ZA VIJANA ZINAWEZA KUSIKIKA?

Kura Yetu
Kura Yetu
Dec 6, 2019 · 3 min read

Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na jarida la Youth Voices au kwa kiswahili Sauti za vijana mwaka 2016 wastani wa umri wa watanzania ni miaka 17. Hii taarifa inaonyesha ya kwamba ⅕ ya watanzania ni vijana wenye umri kati ya miaka 15–24 . Chakusikitisha ni kwamba vijana wengi hapa nchini Tanzania wanaonekana kukata tamaa na kupoteza imani kabisa na nafasi yao katika kuleta mabadiriko katika nchi ya Tanzania kupitia kura zao.Kwa namna moja au nyingine serikali imechangia sana katika kukua kwa dhana hii. Moja ya masuala yanayopendekezwa na sera ya vijana na maendeleo ya mwaka 2007 ni kuudwa kwa Baraza la Taifa la Vijana.

Mwaka 2012 miaka 8 baadae bunge liliafiki kutengenezwa kwa mswada kwa ajili ya lengo hilo na mwaka 2015 sheria ya Baraza la Taifa la vijana lakini hadi sasa hakuna maendeleo mapya. Hivyo basi serikali imeshindwa kuwapa vijana jukwaa lao binafsi lililoundwa na vijana kwa ajili ya vijana.

Kwa hali hii msaada uliobaki kwa ajili ya muongozo wa vijana ni nguvu ya vijana wenyewe binafsi, mashirika binafsi na asasi za kijamii za vijana. Nguvu hizi zinahitaji kuelekezwa kwenye kuchochea utambuzi wa majukumu na haki za kiraia kwa watu binafsi na vikundi kwa mujibu wa sheria. Hii ni kwa ajili ya kusambaza elimu ya kupiga kura na uraia ili kuhimiza vijana wajitokeze kupiga kura na kugombea nafasi za uogozi serikalini.

Kuwepo kwa programu za kuelimisha vijana masuala ya uraia kutasaidia kuwapa vijana uwezo wa kutafsiri sera, itikadi na miongozo ya vyama vya siasa kuwa matendo. Ufahamu huu utaongeza ufuatiliaji wa utendaji wa viongozi waliowachagua kwakufuatilia naoma gani wanatimiza ahadi walizotoa katika kampeni zao za uchaguzi. Uwezo miongoni mwa vijana utawahimiza viongozi walio wachagua kuongeza uwajibikaji katika vipindi vyao vya utumishi.

Jambo hili pia litawezesha ufuatiliaji makini na maamuzi bora na hivyo kubadilisha malalamiko ya vijana kutoka kelele kinazoweza kuzibiwa masikio kirahisi na viongozi, kuwa sauti shupavu zenye kujiamini zinazodai kusikilizwa na pia mabadiliko chanya.

Katika chaguzi za mwaka 2015–2020 taasisi ya Restless Development pamoja na wadau wake waliandaa Ajenda ya vijana ikiwa imekusanya maomi ya vijana mbalimbali Tanzania. Ndani ya Ajenda ya vijana kiliwekwa mapendekezo ya maeneo ya sera yanayo wahusu vijana, pia ilikuwa chombo cha kuchochea vijana kushiriki kwenye siasa na kupaza sauti juu ya mambo yanayowapa wasiwasi juu ya hali ya kisiasa nchini.

Uwepo wa Ajenda ya vijana unapaza sauti za vijana na kutoa muongozo wa maeneo nyeti katika maedeleo ya vijana kwa kukusanya nguvu pasipo na vivuli vya kisiasa. Inawapa vijana kauli moja na hivyo kuziba mianya ya marumbano ya hoja na kualika vyama vya siasa kwenye meza ya majadiliano.

Kwa hali iliyopo sasa sauti za vijana ni hafifu kwani bado sauti za vijana zinatumika kama vyombo vya kupitisha viongozi wakubwa. Vijana wengi hatujiamini na hatuaminiani, ushiriki wa mikutano ya maendeleo ya mitaa na vijiji ni mdogo sana. Baadhi ya vijana wanaotaka kugombea nafasi za uongozi serikalini wanakosa pesa za kuchukua fomu za kugombea na elimu ya kujiandaa kwa sera na kampeni.

Lakini tumaini bado lipo endapo tutaweza kutengeneza umoja wa vijana wenye sauti moja. Taasisi binafsi, vyama vya siasa na serikali tunaweza kushirikiana kutoa elimu za kiraia kuwawezesha vijana kuipata uwezo wa kichanganua sera na kujifunza misingi ya uongozi bora. Vijana wakiwekewa misingi ya kutambua, uzalendo, dhima za uongozi na uvumilivu wa kisiasa sauti zao zitasikilizwa na kuleta mabadiliko.

Tusiishie hapo misingi hii ya URAIA HAI inatakiwa kuchochewa tokea shule za misingi, sio kwa maneno bali kwa vitendo kuwaandaa vijana wa kesho kwa kutengeneza serikali za shule, kugombea nafasi za uongozi kupiga kura na kuchagua viongozi wao wenyewe kwa hatua na mujibu wa sheria za katiba walizotengeneza wenyewe

Kura Yetu

Written by

Kura Yetu

Our intervention addresses low civic engagement by allowing youth to register, speak up, run, observe, vote, follow up and network.

More From Medium

Also tagged Governance

Also tagged Elections

Also tagged Elections

Apr 9 · 4 min read

5

Welcome to a place where words matter. On Medium, smart voices and original ideas take center stage - with no ads in sight. Watch
Follow all the topics you care about, and we’ll deliver the best stories for you to your homepage and inbox. Explore
Get unlimited access to the best stories on Medium — and support writers while you’re at it. Just $5/month. Upgrade