Azaki na matumizi ya vyombo vya habari

Marcela Lungu
Nov 4 · 2 min read

Matumizi ya vyombo vya habari kwa upande wa Azaki yanaongezeka kwa kasi sana ;Vyombo vya habari ni daraja Kubwa kati ya Jamii na Azaki lakini Bado kunauhitaji wa Azaki kujengewa uwezo kuimarisha uhusiano na vyombo vya habari maana Mihimiri hii miwili huleta mabadiliko makubwa katika Jamii.

Changamoto kama vile gharama,kujiandaa bado ni kikwazo katika mahusiano ya Azaki na Vyombo vya habari.

Aidha inatakiwa kujenga mahusiano endelevu kwa kutengeneza Mpango Mkakati wa pamoja kati Azaki na vyombo vya habari.

Internews Tanzania kwa kutambua umuhimu wa Mahusiano kati ya. Azaki na Vyombo vya habari imeandaa mafunzo ya siku 5 kwa Azaki zaidi 5 Kutoka Tanzanzia Bara na Zanzibar kwa lengo la kujengea uwezo na ufanisi kwa Azaki kubadilisha Jamii kwa kutumia vyombo vya habari

Washiriki wa mafunzo wameweza kuelezea umuhimu wa Vyombo vya habari katika kutangaza kazi za Azaki,kubadilisha Jamii na kuleta maendeleo.Aidha kukuwa kwa kasi kwa Mitandao ya Jamii na “newmedia”imesaidia zaidi AZaki kufikisha taarifa kwa watu wengi n muda mfupi “tunatupia mitandao ya kijamii kutoa taarifa mbalimbali kwa umma”Soko kutoka MPC.

Mafunzo ya internews yanalenga zaidi kuboresha habari na kuleta mabadiliko katika Azaki na vyombo vya habari.

Welcome to a place where words matter. On Medium, smart voices and original ideas take center stage - with no ads in sight. Watch
Follow all the topics you care about, and we’ll deliver the best stories for you to your homepage and inbox. Explore
Get unlimited access to the best stories on Medium — and support writers while you’re at it. Just $5/month. Upgrade