Jinsi MAABARA za kupima madini zinavyowatajilisha wachimbaji wa DHAHABU Tanzania

Johansen
4 min readJun 19, 2023

--

Jengo la maabara kwa muonekano wa nje
Jengo la maabara kwa muonekano wa nje

Ilikuwa Mwaka 2017 Baada ya kumaliza chuo (Shahada ya jiologia), Nilianza kufanya kazi katika kampuni (Maabara) mbalimbali za upimaji wa sampuli za mawe, udongo na aina nyinginezo nikiwa kama (Laboratory Geologist).
Tangu wakati huo nimekuwa nikifanya tafiti mbalimbali na kujifunza kutoka kwa wachimbaji wa madini hasa ya dhahabu (wachimbaji wadogo na wachimbaji wa kati)
Haya ni maoni kulingana na utafiti wangu nilioufanya kwa miaka mitano Jinsi hizi maabara za kupima madini zilivyosaidia na kuboresha teknolojia ya uchimbaji hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

MACHIMBO YALIYOPO TANZANIA

Tanzania pamoja na afrika mashariki kwa ujumla tumebahatika kuwa na kiwango kikubwa cha madini katika ardhi zetu.
Madini yanayopatikana kwa wingi ni (Metalic minerals) Dhahabu, Copper, chuma, Nikel, Zinc, Lithium, Tin, lead na mengineyo
Pamoja na madini mengine ya vito kama Diamond, Tinzanite, Rubi nk

Hii makala nitazungumzia madini ya dhahabu na copper (Shaba)

Vipande vya madini ya dhahabu

WACHIMBAJI NI AKINA NANI

Tanzania kuna wachimbaji wa aina tatu

Wachimbaji wadogo — Wanatumia njia za asili za kuchimba madini
Wachimbaji wa kati — Wanatumia njia za kisasa kuchimba madini
Wachimbaji wakubwa — Wanatumia njia za kisasa na mitambo mikubwa kuvhimba madini

Wachimbaji wanavyofanya kazi zao

Kwanza kabisa huwa wanaanza na utafiti wa maeneo (Exprolation) yanayodhaniwa kuwa na madini ya dhahabu. Wanachukua sampuli (Sample) kutoka katika hayo maeneo.
Hizo sampuli zinapelekwa maabara kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kwa kuangalia kiwango cha madini kilichopo

Aina za sample ni
Sample za mawe (Rock sample)
Sample za udongo
Sample za maji
Sample za mimea

Mikoa inayoongoza kwa uchimbaji wa dhahabu Tanzania

  1. Geita
  2. Songwe
  3. Mbeya
  4. Shinyanga
  5. Katavi
  6. Tabora
  7. Mara
  8. Mwanza

MAABARA za kupima madini zinavyofanya kazi

  1. Sample kupokelewa

Mchimbaji anapeleka sample yake maabara kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya madini yaliyopo katika hiyo sampuli.
Sample yake itapokelewa ofisini kwa ajili ya kusajiliwa na kugaguliwa.

Reception sign

2. Sample kuandaliwa (Sample preparation)
Baada ya sample kupokelewa inapelekwa sehemu maalumu kwa ajili ya maandalizi kama kuikausha, kuifanyia sampling na kuiweka sawa kwa ajili ya vipimo vinavyofata
Hapa sample inatoka ikiwa katika hali salama kwa ajili ya kufanyiwa hatua zinazofuata

Sample prep area

3. Crushing and pulvarizing

Sample mgumu ambazo sio za udongo, huwa zinapitishwa katika hii hatua kwa ajili ya kufanyiwa utaratibu wa kupunguza ukubwa pamoja na kusagwa kwa vifaa maalumu ili kupata sampuli ya unga ambayo inaruhusiwa kufanyiwa kazi na vipimo

Crushing and pulvarizing

4. Weighing

Hii ni htua ambayo sampuli iliyoandaliwa inapitishwa kwa ajili ya kuchukua kiwango kidogo cha sampuli kwa ajili ya kuchukua vipimo.
Sampuli inawekwa katika vifaa maalumu vya maabala kwa ajili ya kuchanganya na kemikali nyingine za kuonesha kiwango cha madini yaliyopo katika huo udongo

5. Fire assay na Digestion
Hizi zimegawanyika sehemu mbili
Frire assay ambapo sampuli inachomwa kwa moto mkubwa kutoa uchafu na kubakiza madini yanayotakiwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo

Digestion ni sampuli inachanganywa na kemikali za maji kuweza kuyeyusha madini yaliyopo katika sampuli.

Fire assay na Digestion

6. AAS FINISH

Hii ni hatua ya mwisho kwa upande wa maabara, ambayo ni kusoma sampuli katika mashine maalumu ziitwazo Atomic Absorption Spectrophotometer (AAS) kwa ajili ya kutmbua kiwango cha madini kilichopo katika hizo sampuli

Hizi ni baadhi ya picha mbalimbali za AAS

Different types of AAS

7. Sample reporting

Hii ni hatua ya mwisho kabisa ya kuandaa majibu ya mchimbaji na kumpatia ripoti kamili ya kilichopo katika sampuli yake
Kuna ofisi maalumu kwa ajili ya kutoa majibu

Reporting office

8. Hitimisho
Hizi hatua zote zinachukua masaa matatu mpaka sita, kulingana na wingi wa kazi zinazipelekwa maabala

Hatua zote kwenye picha moja

Kwanini wachimbaji wanatakiwa kupeleka sampuli zao maabara?

Hii makala inaendelea………
Kwa mawasiliano email yangu ni hii bofya hapa whatsapp

--

--

Johansen

blockchain and Cryptocurrency researcher and content writer