Je? Kifo cha lugha ya Swahili kinakaribia katika Afrika Mashariki?

Imekuwa muda mrefu tangu niandike kwa lugha ya Swahili. Kwanini basi ninaiandika ujumbe huu katika lughya inayotumika zaidi na watu katika Africa Mashariki? Sababu ni mbili. Katika utafiti wangu unaozingatia matumizi ya mitandao ya kijammi na vyombo vya habari kwa jumla, nimetizama ya kwamba lugha inayotumika zaidi katika mtandao wa internet ni Kingereza. Utafiti uliofanywa na wenzangu katika chuo kituu cha Oxford, uliangazia kua lugha ya Kiingereza inangoza katika matumizi ya tovuti ya Wikipedia na sana sana michango katika tovuti hio yamefanywa kwa lugha ya Kiingereza. Picha inayofuatia inaonyesha Kiingereza kinatumika zaidi Africa Masharikini. Mbona Africa Mashariki na Africa kwa jumla hawatumii lugha zao za asili? Katika ustadi wa matumizi ya internet, lugha inachangia pakubwa vile jamii inatumia mtandao huo. Kwa mfano, wale wasiojua Kiingereza wanapata wakati mgumu kupata habari.

Sababu ya pili ni kuwa, juzi juzi nilikuwa nikitizama runinga ambapo nikamwona mwandishi Ngugi Wa Thiong’o akihimiza kuwa sisi kama Waafrika tunafaa tukizingatia utumizi wa lugha zetu za kiasili. Alisisitiza kuwa Kiingereza ni lugha ilioletewa na wakoloni ambao walifananisha lugha zetu za asili na lugha za watu walio nyuma kijamii.

Ndipo wazo likanipita, nikajiuliza. Je? Katika miaka hamsini au mia moja inayokuja, Kiswahili kama lugha kitakua ama kitakuwa kimeangamia? Katika uchambuzi wangu, maoni yangu ni kwamba nchi ya Tanzania itakuwa na wachambuzi wengi wanotumia lugha ya asili ya Kiswahili. Tayari, katika mitandao ya jamii, kama vile Twitter na Facebook, ni Watanzania sana sana wanaotumia lugha ya Swahili. Kuna blogu tofauti tofauti zinazotumia Kiswahili kama lugha ya maandishi.

Nikweli ya kuwa Nchi ya Tanzania inatumia Kiswahili zaidi na pia mfumo wao wa shule unatingatia matumizi ya Kiswahili kuliko Kiingereza. Kenya inatofautiana na Tanzania katika mfumo wa shula ambapo Kiingereza kinazingatiwa. Kiswahili nchini Kenya kinaoneka kama lugha nyingine, mmoja ya lugha zingine tunazotumia lakini Kiingereza kinapewa kipao umbele. Hii imesababisha matumizi tofauti tofauti na kuchipuka kwa lugha zingine kama vile lugha ya Sheng’. Sheng’ ni lugha isiokuwa na sheria ya aina yeyote na inazidi kuvuma nchini Kenya sana sana Nairobi.

Wataalamu wengi nchini Kenya wanamaoni ya kua utumizi wa Kiingereza utaiweka Kenya pahali pema katika juhudi mbali mbali na mataifa mengine duniani. Katiba biashara, katika masomo ya Kisayansi, ni baadhi ya sababu wanazozitoa. Tayari lugha ya kiasili ya Ichamus na Elmolo yanayotumika karibu na ziwa la Turkana yako karibu kuangamia. Je, unafikiri miaka hamsini zinazokuja Kiswahili kitakuwa kimeaangamia?

One clap, two clap, three clap, forty?

By clapping more or less, you can signal to us which stories really stand out.