what Agriforum deals:

Agri-Busi forum (Agriculture and business forum) ni Mtandao ambao unajishughulisha na kutoa Elimu ya ujasiriamali, kilimo, biashara na ushauri nasaha kwa makundi maalumu, pamoja na wajasiriamali wadogo. Vijana wengi wanakua na dhana potofu kwamba tatizo la umasikini linatokana na ukosefu wa pesa au mitaji peke yake. 
Lakin sisi tunamtizamo tofauti, kama tatizo la umasikini lingekuwa ni ukosefu wa fedha kuna matajiri wawili kule Marekani, Donald Trump na Robert Kiyosaki wamesema kwamba wangejitolea kuwagawia watu pesa lakini katika utafiti wao wamegundua kwamba hata ukimpa mtu pesa atatumia zikiisha atarudi tena kuja kuomba,
 hivyo mbinu hiyo siyo endelevu inamfanya huyu anayeomba kuwa tegemezi na kuzidi kuwa masikini ndio maana tunasema sasa ni wakate wa kupeana nyavu ili tukavue samaki ili tuache kutegemea kupewa samaki. Vivyo hivyo katika kumkomboa mtu kutoka kwenye umasikini unatakiwa kupatia elimu ya ujasiriamali .

MALENGO
Malengo yatu ni kutoa huduma bora za ushauri kwa vijana na wafanyabiashara wadogo ili waweze kujiendesha katika shughuli zao za ushalishaji kwa ufanisi.

DIRA YETU.
Tunaamini kwamba matatizo yanayozuia maendeleo ya Wajasiriamali Tanzania ni pamoja na ukosefu wa mitaji na elimu ya biashara,hivyo lengo letu ni kuhakikisha tuanatoa elimu ya biashara na Kilimo na uendeshaji wake.
MALENGO YETU YA BAADAE
1.Kutoa ushauri wa Wafanyabiashara wadogo , na wakina mama katka vikundi vyao.
2.Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili..
3.Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara.
4.Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu..
5.Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni.
6.Kuandaa nyaraka za Tenda.
7.Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi.
8.Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
9.Kutunga vitabu vya ujasiriamali na biashara ili kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi.
10.Kutoa ushauri nasaha na mafunzo kwa wanafunzi.

MIPANGO YETU YA BAADAE
Kuimarisha biashara yetu ili tuweze kuenea maeneo yote ya Tanzania.
Admitted by ceo@agriforumtanzania
Agri.busiforum@yahoo.com
 Tanzania