Matukio chanya ya kiuchumi mwaka 2022 katika Taasisi mbali mbali Tanzania.

lukelo Ngajilo
10 min readDec 30, 2022

--

Ndugu msomaji, hongera kwa kuwa na uhai na pumzi maana kama waisoma nakala hii, umejaliwa kuwa na uhai, ni raha ilioje nimekusanya matukio machache ya muhimu yanaweza kukusaidia wewe kutafakari mwaka 2023.

Taasisi za kifedha

Hifadhi ya fedha ya kigeni imeshuka, je ? ni vizuri au vibaya ?, kwa upande wangu naona ni “vibaya”, kwa wale watu wenye akiba ya fedha za kigeni kwenye akaunti zao binafsi au mifukoni watapata faida.

Kwa , nazo kwa sababu fedha yetu inaweza kushuka thamani kidogo dhidi ya fedha za kigeni, hata hivyo tukiangalia vizurii unaweza kuona fedha zetu zimeanza kushuka tayari.

Hata hivyo kwakuanza kabisa Benki za Tanzania ziliopewa pumzi !, je zilikuwa zimekufa? sii jui, lakini pumzi waliyopewa benki zimesaidia zifanye vizuri ? ndio, je pumzi waliyopewa ni nini ?, mimi pia sijui. lakini utajionea kabisa iyo pumzi waliyo pewa imefanya kazi kubwa sana. “Mama anaupiga mwingi” na mimi pia angenipa iyo pumzi ningefurahi sana.

Benki kuu

Serikali ya Tanzania kupitia Benki kuu huwa inakopa kwa taasisi na wananchi wake ili iweze kujiendesha katika mwaka husika wa Serikali, kila jumatano ya kila wiki ya mwaka mzima huwa hatifungani zinauzwa kwa njia ya mnada.

Lakini kwa miaka zaidi aya mitano licha ya hatifungani zetu kuwa na riba kubwa sana, zilikuwa zinanunuliwa kwa bei ya chini.

Serikali ikiwa inauza hatifungani kwa bei ya milimo moja lakini ilikuwa inanunuliwa kwa bei ya laki tisa, yani wanunuzi walikuwa wachache sana na walioto ofa ndogo sana sokoni na cha ajabu zaidi mwaka huu January kulitokea na mapinduzi makubwa kuliko.

Hata hivyo kuna uwezakano Wakinga ndiyo waolijanzaa huu mkeka maana wale wakinga wakisha uza misonobari (pines) zao kule makete haraka tuh wanakuwa na fedha kibao watu wa mapemberoo wako na mabumunda yao.

Mabumunda — mikate ya kikinga inatengenezwa na unga wa ngano haiwekwi amila ukinywa asubuhi na chai ya moto unasubiria chakula cha jioni.

Mapemberoo — hii ni salamu ya kikinga.

Watu na taasisi mbali mbali zili toa Ofa (Zabuni) lakini zilikataliwa zaidia ya bilioni mia tano. zilikataliwa lakini kwenye uchumi hii ni hatari sana ! , kwa sababu wananchi na taasisi hazioni njia nyingine za kufanya uwekezaji na biashara na kuwekeza kwenye hatifungani. kwaiyo pesa inakuwa haiko mitaani. kwenye swala la uchumi ni vizuri watu kuanzisha biashara na kampuni kuliko kuwekekeza iyo pesa kwenye hatifungani.

Baada ya serikali kuona wawekezaji wana shauku kubwa ndipo serikali ikaamua punguza riba ili shauku ya wawekezaji ipungue. Kuna ule msemo unaosema “kiu ya maji kamwe haimalizwi kwa soda” basi mijadala hiyo ilianza kurushwa magazetini na hazikupita siku nyingi Serikali iliamua kushusha riba, hivyo basi hadi leo hii 29/12/2022 bado wanunuzi ni wengi.

Hata hivyo mkeka ni kama unavyoona hapa juu, mkeka wa zamani na mkeka mpyaa riba iliyopo bado ni kubwa sana, ndugu msomaji kama ukipata fedha za kutosha fanya namna ununue hatifungani.

BLOCKCHAIN

Vilevile Benki Kuu na Wizara ya fedha kupitia Waziri Mwigulu Nchemba walionesha nia ya kuanza matumizi ya sarafu za mtandaoni au Cryptocurrency hapa Tanzania. Je, walifikia wapi na wapo wapi? Mimi pia nashindwa kupata jibu.

Benki binafsi

Tukio lingine la la liliogonga vichwa vya habari ni pamoja na benki binafsi kurekodi faida lukuki, ni pamoja na benki ya NMB na benki zingine. Huku NMB ikiongoza kwa kutengeneza faida ya bilioni 209 ikifwatiwa na CRDB na benki zingine.

Katikati ya mwaka huu wa fedha benki zilipata faida kubwa sana, hili ni swala chanya sana katika uchumi wetu, maana benki zetu zinafanya biashara na kupata faida maana watu wanakopa na kurudisha fedha, hili ni swala linalo leta afya katika nchi yetu.

Kwa faida hizi kuna uwezekano wana hisa kupata magawio makubwa mwakani.

Lakini pia mwaka huu benki mbalimbali zimeweza kukusanya mitaji kwakuuza hatifungani zilizo tambulishwa sokoni hivi karibuni, benki ya NMB nayo ilitambulisha sokoni bond yake iitwayo Jasiri Bond, nayo ilikuwa oversubscribed hii imeonesha kwamba wananchi wana hela yani (mtaani pesa zipoo) .

Benki hii ya NMB wameweza kufungua akaunti za kibenki zaidi kuliko malengo yao kwa mwaka huu wa fedha yani mwaka 2022, zaidia ya akaunti milioni moja zimefunguliwa na hawa ni wateja wapyaaa !.

kuwa oversubscribed — maana yake yani wamekusanya pesa kuzidi malengo.

Lakini pia siyo benki ya NMB pekee, pia KCB na NBC nao bonds zao zilizo tangazwa zilikuwa (oversubscribed ) kitendo hiki kinaonesha watu wengi wanafedha mtaani na NBC imetokea kuwa (oversubscribed) ya bilioni nane (8) yani wao lengo lao lilikuwa bilioni 30 lakini bilioni nane zimezidi.

Zaidi ya miaka mitano iliyopita sijawahi kuona matukio kama haya hili inamaanisha uchumi umeimarika.

Lakini pia kongole (hongera) sana kwa aliye waambia NBC wafanye ufadhili katika ligi ya mpira ligi kuu kwani imewarudisha sokoni, mana ilipotea kabisa kwenye rada, naamini mwakani itapata matokeo chanya zaidi.

Pia, taasisi za fedha (YETU )ya kukopesha ipo katika uangalizi maalumu wa Benki kuu ya Tanzania taasisi hii inahusika na kutoa mikopo, taarifa zake za fedha zilizotoka zilioneSha kabisa mikopo waliyotoa ni mingi kuliko pesa walizo kusanya kiufupi ilikuwa inaelekea kufilisika kwa ninavyo dhani.

Benki kuu ya Tanzania wakaona waiweke katika uangalizi maalumu kwa kipindi fulani hivyo basi tuwe wavumilivu tusubirie tuone panapovuja pataonekana.

Kuanzishwa kwa mfuko mwingine wa uwekezaji mfuko huu unaitwa Faida Fund uko chini ya Watumishi Housing Investment.

SOKO LA HISA

Vilevile, soko letu la hisa halikuwa nyuma hisa za kampuni nyingi za Tanzania zimefanya vizuri sana pia iliandikwa magazetini, lakini ukiona imeandikwa magazetini ujue tayari waliokuwa wamewekeza washapiga pesa au umechelewa, maana hiko ni kipindi cha kuuza hisa watu wame nunua muda mrefu yani hisa zilikuwa chini lakini wakitangaza zinakuwa zimeshapanda tayari.

Kampuni ya CRDB imewahi kuwa na bei ya 400 mwaka 2014/2015 lakini haijawahi tokea tena tangu kipindi iko, mwaka huu ndio imesogea mpaka 385, je mwakani itapanda zaidi au itashuka “Mama anaupiga mwingi”.

JE UNA WAKUMBUKA JATU ?

“JENGA AFYA TUKOMEZA UMASKINI”

Hawa ni wazawa walio tunikiwa shahada mbali mbali katika chuo kikuu cha dar es salaam, vijana wakajiajiri wakaona yafaa kabisa kufanya mabadiliko katika kilimo wakajiajili kama viongozi wetu wanavyoomba kila siku “tujiajili vijana” hawa jamaa ndio walikuwa wa kwanza kuja na “BLOCK FARMING” wakachangisha zaidi ya bilioni 5.1.

Kijana huyu wa miaka thelathini na mbili (32) (rich and young) alikusanya pesa za watu kibao sana ili waweze kufanya block farming, kwa sababu ili kilimo ufanye vizuri unahitaji mtaji mkubwa hawa jamaa wakakusanya mtaji kwa wananchi lakini haikuwa hivyo pekee waliweka kampuni yao katika soko la hisa, aiseeh ilikuwa moja ya hisa inayofanya vizuri walikuwa washakunya mabilioni ya pesa, lakini kutoka na navyoona walingia tamaa kubwa wakaanza kukusanya fedha nje ya soko wanadaiwa kukusanya BILIONI TANO (5.1) kwa njia isiyo sahihi.

Lakini JATU wapewe pongezi walifanya pia serikali ifanye (adoption) ya BLOCK FARMING, je unakumbuka mashamba ya dodoma yaliyo zinduliwa na Waziri wa Kilimo kwajili ya vijana, je wewe kama kijana umepata shamba la kulima?.

VIJANA HAWAJAKUBALI KUBAKI NYUMA !!

Startups ni kampuni changa zinazo anza kwa nguvu na kasi kutoa huduma au bidhaa katika jamii.

Nakurudisha nyuma kidogo mwaka 1939 -1945 kipindi kuliko kuwa kulikuwa na vita vya pili ya dunia mjerumani ndiye alikuwa ame advance sana kiteknolojia ya kivita na vingine kuliko muingereza.

Kiufupi Mwingereza hakua na ndege za kivita, mawasiliano yake yalikuwa ya simu za mezani kiasi kwamba unaweza kata nyaya na asiwasiliane, lakini mwingereza alikuwa katika kipindi cha kufa au kujiokoa.

Wazungu wanasema “do or die” baada ya hapa chimbuko la startups lilipoanzia kwa mara ya kwanza kwani binadamu aligundua kompyuta(computer) ya kwanza ilikuwa inaweza saidia kudadavua mawasiliano ya siri ya Mjerumani hapo yakasaidia ujerumani kupigwa katika vita ile.

Tanzania kumekuwa na kampuni changa zenye kuleta mambo chanya katika jamii yetu lakini ili ziweze kugusa jamii yetu kwa ukubwa inabidi ziwe na mtaji wakutosha kampuni hizi huwa zinaomba mtaji kwa Angel investors (hawa ni wawekezaji wa mwanzoni kabisa) ili wapate mtaji wakufanya uendeshaji (operations) bila shida.

Katika mwaka 2022 vijana wa Tanzania hawakubaki nyuma kati ya kampuni chache zilizo weza kupata fedha kutoka kwa wawekezaji ni RAMANI, vijana hawa ni vijana wenye (exposure) kubwa sana wameshafanya kazi kwenye makampuni makubwa ya teknolojia Nchi za Nje, kama vile kampuni yao ya RAMANI ningekuwa sina jambo la kufanya ningeenda hata kujitolea katika kampuni yao maana hutotoka bure kabisa, labda usiwe mtu wakujifunza.

Wana mifumo ya kidigitali inayorahisisha

  • Manunuzi
  • inventory
  • financing

kutokana na umahili wao wamekusanya fedha Bilioni 74.6 TZS, jamani hii ni pesa nyingi sana hebu fikiria (just imagine) watu wanakuamini na kukupatia fedha zao, ni dhahili kwamba inaaminika kuwa utafanya vitu vikubwa maana watu pesa yao watauliza imetumika kufanya nini?

SWAHILIES

Vijana wengine hawa wamesoma hapa Tanzania wenyewe wanasema wenyewe ni “WORLD CLASS” nao hawakuwa nyuma wana mifumo yao inaitwa swahilies na kuzaa zinatoa huduma zifuatazo

  • Kukusanya malipo kidigitali kutoka kwa wateja endapo mteja anataka kulipia bidhaa kidogo kidogo kupitia Swahilies
  • Pia wanatunza kumbukumbu za manunuzi na mauzo ya watu wanao miliki biashara kupitia mfumo wao unaitwa Kuuza
  • Wanarahisisha malipo ya mtandaoni(online) kwa kutoa APIs(application programming interface) za kulipia malipo kidigitali kwa kiswahili, sijui tafasiri yake kwa kiswahili, kiswahili kigumu sana

kiukweli ni vijana wazuri sana wana tia msukumo (inspire) sana, hawa vijana wameweza kukusanya zaidi ya dola 50,000 na kila nikiwaza wanafanya nikose usingizi.

Nitaelezea story yao kidogo ninayo ijua,

Hawa ni vijana walikuwa na mfumo wa (ecommerce) unaitwa swahilies baada ya kufanya biashara na kutathmini wakagundua hakuna kitu wanapata na biashara ni ngumu sana maana shida iko kwenye usambazaji wa bidhaa (logistics) mtu yupo gongo la mboto anaagiza kitu kariakoo, faida yote inaishia kwenye usafiri ndio wakafanya pivoting (kubadilisha mfumo wa biashara) ni mfano mzuri wa vijana wanao pambana bila kuchoka.

EAST AFRICA FRUITS

Huwa huoni ata malori yana beba viazi vingi (kama unaishi Dar es salaam) na matunda kila asubuhi basi jua ni kijana wa kitanzania ndo mwenye kampuni inasambaza hapa Jijini dar es salaam kila siku, ni simu mojaa tu, hao wanakuja. Nao waliweza kukusanya dola 300,000.

“Wauza viazi na matunda”

Ndugu msomaji wa nakala hii kwa mwaka unaofwata pambana upate (exposure) sana. Utafanya kazi sana lakini kama unakosa exposure hakuna kitu unafanya utachelewa sana, ukipata exposure mambo yatakuwa mepesi.

Lakini pia mimi kama mwandishi natafuta exposure hakikisha unaishi na kufanya kazi ki “WORLDCLASS”, exposure sio kwenda nje ya nchi maana kuna walioenda lakini ni kama walikuwepo Tanzania nasisi ndani tu, hawana jipyaa.

“kusoma nchi za njee sio kupata exposure”

kipekee sana mwaka 2023 nitakuwa natafuta exposure sana.

Kumbuka;

World Bank wanakwambia Tanzania haina wasomi wa kutosha kuweza ku endesha uchumi wa nchi. Je ni waongo ? au wamemaanisha nini ?, wanatojora sisi jobless.

Hata hivyo alisikika muhenga mmoja akisema “kidole kimoja hakivunji chawa” , hivyo basi tufanye kazi kwa kushirikiana ile tuweze kufikia malengo.

Jambo zuri na lakutia moyo ni kwamba Tanzania inakuwa kiuchumi haraka sana kuliko CHINA “Tafakari chukua hatua”.

Tanzania bado ina rasilimali (resources) nyingi sana maanai ukikosa hapa kuzipata nchi zingine ni adimu na ngumu sana.

Tanzania ni nchi yenye amani sana !!

Ndugu msomaji, Dar es salaam inatarajiwa kuwa Mega city, je umejiandaaje sio leo wa kesho lakini ni karibuni hapa.

Msomaji, kama upo Dar e salaam jua kwamba KARIAKOO ndo soko lenye ukubwa zaidi Africa mashariki usije sema huku ambiwa !, yani watu kutoka Rwanda, Kongo, Kenya, Uganda ,Burundi , Zambia, Malawi wanatumia soko la kariakoo hata watu wa visiwa vya Comoro.

Lakini pia, Tanzania Bado ni nchi changa sana katika nyanja mbali mbali. yani hata ukisema soko bado ni changa sana !.

Tanzania ina makabila mengi zaidi ya mia na ishirini na tano (125) lakini hakuna maswala ya ukabila kabisa, ni nchi yenye upendo na amani, ukiangalia Kenya makabila si mengi sana sidhani kama ni zaidi ya kumi (10) lakini unaweza kuona ni jinsi gani wanavyo vurugana, Rwanda pia vilevile.

Lakini pia Nchi yenye bahati sana mfano mzuri ukiangalia kwenye soko letu la hisa wauzaji na wanunuzi zaidi ya asilimia hamsini sio watanzania.

Tukiangalia kwa undani Tanzania katika soko la hisa kuna watu wanapata kubwa.

https://younginvestorsforum.or.tz/ hii ni forum ya vijana wa kitanzania wanafundisha uwekezaji bure hakuna na haijawahi tokea dunia nzima huko dunia watu wanalipia.

Enjoy while it lasts.

Lemutuzii anasema “BOYEE KANYAGA TWENDEEE, TUMECHELEWA”

Matukio ni mengi haya ni machache.

Author Lukelo Ngajilo Email ; ngajilol@gmail.com.

--

--