How to fix Bongo Movie: Punguza idadi ya filamu zinazozalishwa.

Nadhani ni kweli soko la filamu limedorora, kila mtu anasema hivyo, kuanzia waigizaji hadi watazamaji,wahusika wa tasnia wakisema basi itakuwa ni kweli. Kujua tatizo ni nini, labda tuone mwanzoni kwa nini soko lilikuwa.

Nini kilikuza soko la filamu hapo mwanzo?

Ukiniuliza mimi nitasema kwamba mara zote watu wanataka burudani kutoka nyumbani, filamu yenye mazingira na maudhui yanayofanana na yanayomhusu mtazamaji basi ndo inakubalika zaidi. Mfano, kabla ya Bongo Movie, Filamu za Nigeria ndo zilikuja kwa kasi, nakumbuka mama yangu alikuja na filamu mpya ya Nigeria kila siku jioni, alizikubali movie za Nigeria kuliko za Marekani (Rambo, Commando etc..) kwa sababu atleast zilianza kufanana na mazingira yake halisi. Zilipokuja Bongo Movie zikawa ni mbadala wa Nigerian movies, basi kilichotokea baada ya hapo ni bongo movie kupiku movie za Nigeria kwa Tanzania.

Tatizo ni nini kwa sasa:

Masoko ya bidhaa kuyumba na kutengemaa ni kawaida, ishu ni pale kuanguka kwa soko kunapoendelea kwa miaka kadhaa , hapo ujue kuna ishu tofauti imetokea, hivyo nawasilisha kwamba hili ndo tatizo;

Bongo movie hawajasoma mabadiliko ya wakati:
Bongo movie ilipoanza, watanzania walikuwa na vyanzo vichache sana vya burudani, utasikiliza redio, utasoma gazeti la Shigongo au utatazama TV ambapo labda usubiri muda wa Igizo jioni na marudio Jumamosi. Kwa hiyo watu walifurahia na kupokea burudani ya filamu za kiswahili ambazo walizielewa vizuri bila shida ya lugha, pia walielewa mazingira vizuri bila kuchanganywa na mambo madogo kwa mfano kwenye movie ya Nigeria mtu akisema “Naira Elfu moja” ni hela nyingi au chache? kwenye bongo movie mtu akisema ameibiwa laki tano basi wote tunaelewa vizuri.

Kwa sasa ishu ni kwamba mambo yamebadilika, Mtanzania wa sasa ana mamilioni ya vyanzo vya burudani; Whatsapp, maelfu ya page za Instagram na facebook , Mamilioni ya channels za YouTube etc..

Inawezekana mwanzoni uliweza kuuza filamu kwa sababu tu Wema Sepetu au Hemedi yupo kwenye kava na watu wanataka kumuona, sasa hivi huwezi kumpumbaza hivyo kwa sababu anapata Drama zote za wema sepetu kwenye instagram ambako anapata picha mpya na post kila masaa mawili. Pia “drama” za instagram ni entertaining kuliko script yoyote iliyowahi andikwa bongo movie, mwandishi gani atanogesha kuliko matukio ya kwenye mitandao ya jamii kwa sasa. Mteja atanunua bando ya internet kuingia youtube na instagram kabla hajanunua bongo movie.

Okay, so tufafanyaje:

Ulimwengu wa sasa ni wa mitandao na social media, kwenye ulimwengu huu mteja wako muda wote ana notification za whatsapp, Facebook, Instagram, Snapchat etc ambazo zinamwita atumie muda wake huko. kwa hiyo unapomwambia mteja atazame Movie yako ujue kwamba inashindana na vyanzo vyote hivyo vya burudani vinavyotaka attention yake.

Tatizo ni kwamba bongo movie ilifanikiwa “at some level” kwa kuzalisha filamu nyingi za ubora wa kawaida au wa chini. Baada ya muda watu wakaanza kuona hazina jipya, hivyo wakapeleka attention yao kwingine.

Unapozalisha filamu mpya, fikiria kushika attention ya watu, Yaani fanya mteja wako ashindwe kuacha impite (Content must be compelling).

Nadhani mambo yafuatayo yanaweza kusaidia kwenda mbele:

1. Zalisha filamu chache zenye ubora:
Research topic ambazo zinazovutia hisia za watu kwa sasa, mfano kwa sasa labda story ya kijana aliyfight muda mrefu na kuja kuwa mtu mkubwa katika jamii na kupendwa na watu huku wengine wakimchukia.
Andika filamu vizuri, tumia muda kuifanya script iwe nzuri na imejitosheleza.

Ajili watu wanojua na wanaopenda wanachofanya, waigizaji, wapiga picha, waongozaji na hata waandaaji wa nguo za wahusika tu.

Taka kuonesha utofauti na kuvutia maongezi ya watu, taka watu waambiane kuhusu filamu yako mpya na watumiane kwenye Whatsapp na mitandao ya jamii.

2. Ufunguzi na promotion.

Fanya ufunguzi wa filamu yako kuwa tukio, Ni vizuri kufungua kwenye ukumbi wa sinema, hii inaipa filamu uzito na watu kuizungumzia. Hii inaweza kuwa event ambayo ina after party baada ya filamu ambapo watu walionunua filamu wanajumuika na waigizaji etc.

3. Zalisha filamu chache.

Mfumo wa kuzalisha filamu nyingi na kupata faida ndogo kwenye kila filamu ulifanya kazi kwa muda, lakini nadhani kwa sasa hautafanikiwa. Zalisha filamu chache kwa mwaka, ziwe bora na nzuri. Hii itasabisha ufunguzi wake na utangazaji wake uwe bora pia.

Hizo ni senti mbili zangu :)