TAARIFA YA MKUTANO MAALUMU WA WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA NA WATANZANIA CHINA

Victoria C Mwanziva
Sep 6, 2018 · 4 min read

Mkutano Maalumu wa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ulifanyika Ubalozi wa Tanzania Beijing tarehe Septemba 2, 2018- ambapo alitumia nafasi hiyo kukutana na Watanzania Wanaofanya Biashara, Wanaofanya Kazi, Wanaosoma na Wanaoishi China.

Mheshimiwa Waziri Mkuu aliambatana na Viongozi wengine ambao walikuwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga; Mhe. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mhe. Rashid Ali Juma, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Viongozi wengine Waandamizi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuja China kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) unaofanyika Beijing, China. Ila akaona ni vema na sahihi akitupa nafasi Watanzania tuliopo China kwa shughuli mbalimbali, uwanja wa kutusikiliza na pia kusikia ujumbe kutoka kwake.

Kwa upande wa Shirikisho la Jumuiya za Watanzania Wanaosoma China (TASAFIC), Tuliwakilishwa vema na Mwenyekiti wetu ndugu Denis Mukama aliyewasilisha hotuba mbele ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo kwa niaba ya Watanzania Wanaosoma China.

Hotuba yake iligusa utambulisho wa Shirikisho letu la TASAFIC, pamoja na changamoto mbalimbali na maono tuliyoyawasilisha kupitia utaratibu ulioratibiwa na Katibu wa TASAFIC hapo awali.

Ushiriki wa Jumuiya za Tasafic Ulikuwa mzuri wa kuridhisha ambapo- TASAFIC Kamati Tendaji iliwakilishwa na Mwenyekiti Ndugu Denis Mukama, Makamu Mwenyekiti Bi Victoria Mwanziva, Muweka Hazina Bi Lucynancy John.

JUMUIYA MBALIMBALI ZILIWAKILISHWA KAMA IFUATAVYO:

Jumuiya ya Beijing inyayoongozwa na Ndugu Kulwa Gamba (Mwenyekiti Beijing).

Jumuiya ya Beijing ilikuwa mwenyeji wetu mkuu wa Shughuli hii, na walikuwa na uwakilishi mzuri kwenye shughuli hii.

Jumuiya ya Harbin iliwakilishwa na Bi Victoria Mwanziva (Makamu Mwenyekiti Harbin, Makamu Mwenyekiti TASAFIC)

Jumuiya ya Henan iliwakilishwa na Bi Phelister Wegesa (Mwenyekiti Henan)

Jumuiuya ya Jilin iliwakilishwa na Mwenyekiti Denis Mukama (Mwenyekiti Jilin, Mwenyekiti TASAFIC)

Jumuiua ya Jinhua iliwakilishwa na Lucynancy John (Muweka Hazina Jinhua, Muweka Hazina TASAFIC)

Jumuiya ya Qingdao iliwakilishwa na Yazid Iddi (Mwenyekiti Qingdao)

Jumuiya ya Shanghai iliwakilishwa na Bi. Angel Richard Kessy, Dafina, Ndugu Charles

Jumuiya ya Shenyang Iliwakilishwa na Ndugu Berrington (Makamu Mwenyekiti Shenyang)

Na Jumuiya ya Tianjin iliwakilishwa na viongozi wao ambao ni Martin Itangaja (Katibu wa kamati ya jamii na michezo), Joyce Ndauka- (Kaimu katibu). Hija Athman (Mwenyekiti kamati ya nidhamu, Sheria na Katiba). Beatrice Mushi- (Katibu kamati ya fedha na Mikopo) Pamoja na wanachama Castro Mwankefu- (Mwanachama), Bahati Gasper Mteti- (Mwanachama)

UJUMBE KUTOKA KWA WAZIRI MKUU:

Mheshimiwa Waziri Mkuu aligusia masuala mengi sana kwenye hotuba yake kwenye mkutano maalumu uliofanyika kati yake na Watanzania waliopo China- Masuala Makuu muhimu yanayotugusa ni kama yafuatayo-

Watanzania tulipo China tudumishe Umoja, kwani Umoja ndio msingi wa mafanikio- amepongeza uwepo wa TASAFIC na amesisitiza sana tuudumishe umoja huu kadri ya uwezo wetu.

Matumizi ya Elimu yetu kwa Manufaa ya Kuinua Tanzania:

Amesisitiza Watanzania tuliopo China- tufanye tafiti mbalimbali za kitaaluma na kuhakikisha kuwa taaluma hizi tuzisomeazo zitakuja kuinua taifa letu la Tanzania.

Juhudi katika masomo- Mheshimiwa Waziri Mkuu amesisitza sana tujitahidi kujituma katika masomo yetu ili tuweze kumaliza tukiwa na ujuzi mzuri kutoka huku China

Mheshimiwa Kassim Majaliwa Kassim ang’oa mzizi wa Mawakala wasio waaminifu kwa kuamuru papo hapo mkutanoni baada ya kusikia kilio cha wanafunzi wengi kuhusiana na masuala ya Mawakala- ameamuru kuwa Mawakala wote wanapaswa kujisajili Wizara ya Elimu waweze kutambulika- na waweze kufanya kazi kwa mipaka ya Wizara ya Elimu. Gharama zao hazipaswi kwenda kuumiza Watanzania katika huduma wazitoazo.

Lakini Watanzania wote wanaopata nafasi za kimasomo kupitia Mawakala wanapaswa kufikishiwa taarifa zao Ubalozini na mawakala hao ili kila Mtanzania anayeingia nchi husika atambulike Ubalozini.

Masuala ya vyeti vya wahitimu kutoka China katika Taaluma mbalimbali;

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Wahitimu wanaohitimu China- wanapaswa kuhakikisha taarifa za kozi zao zipo sahihi ili vyeti vinaporudi Tanzania na kuhakikiwa na TCU ziwe na uhakika haswa kwenye suala la Specialization za kozi zao husika.

Aidha amemuagiza Mheshimiwa Waziri wa Elimu kufuatilia kwa Karibu suala hili.

Aidha Mheshimiwa Waziri Mkuu aligusia kuhusiana na suala la kuendelea kushikamana na Ubalozi, katika hatua zetu zote. Amempongeza sana Mheshimiwa Balozi Kairuki kwa kazi kubwa anayoifanya hapa China.

Salaam nyingi zimewasilishwa kwetu sote na Viongozi waandamizi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliozungumza katika hafla hiyo akiwemo Waziri wa Mambo Nje Mheshimiwa Balozi Augustine Mahiga aliyeainisha historia ya Ushirikiano baina ya China na Tanzania pamoja na umuhimu wa kuutunza umoja wetu huu.

Uongozi wa Shirikisho la Watanzania Wanaosoma China unashukuru sana Ubalozi wa Tanzania nchini China kuandaa hafla hii muhimu ambayo tulipewa fursa ya kushiriki, na kusikia mengi kutoka kwa Waziri Mkuu-

Aidha tunashukuru Uongozi wa Jumuiya ya Beijing Ukiongozwa na Mwenyekiti Ndugu Kulwa Gamba na Wana TZSUB wote kwa upendo wao na umoja wao haswa juu ya mapokezi mazuri ya Wanashirikisho kutoka majimbo mbalimbali waliofikia Beijing kwa ajili ya mkutano huu.

Aidha pia tunashukuru kwa umoja wetu Viongozi na wawakilishi waliojitolea kwa moyo mmoja kushiriki katika Shughuli hii muhimu- kuwakilisha Jumuiya zao na kushiriki kikamilifu na watanzania wenzao katika hafla hii muhimu ambayo ilituleta pamoja na kutupa nafasi ya kujumuika kwa pamoja na kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ya Ustawi ya Jumuiya zetu.

Umoja wetu ndio msingi wa maendeleo na ustawi wetu.

Victoria Mwanziva

Makamu Mwenyekiti Shirikisho la Jumuiya za Watanzania Wanaosoma China (TASAFIC)

Septemba 3, 2018


Originally published at victoriamwanziva.wordpress.com on September 6, 2018.

    Victoria C Mwanziva

    Written by

    MPA-Harbin Institute of Technology. BA (Hons)- Political Science & Public Administration UDSM. A Propagator of Development & Empowerment.

    Welcome to a place where words matter. On Medium, smart voices and original ideas take center stage - with no ads in sight. Watch
    Follow all the topics you care about, and we’ll deliver the best stories for you to your homepage and inbox. Explore
    Get unlimited access to the best stories on Medium — and support writers while you’re at it. Just $5/month. Upgrade