FUATA HATUA HIZI KUWEKA TAARIFA ZA BIASHARA YAKO GOOGLE MAP.

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI
3 min readMay 23, 2019

Kuna faida nyingi na za wazi za kuiweka biashara yako kwenye Google map. mfano ni:

  • Ni bure na uhitaji kulipia gharama yoyote
  • Itasaidia wateja wako kupata taarifa zako za msingi kirahisi pale wanapo kusearch kwenye google. Mfano wa hizo taarifa ni kama namba ya simu, location, picha nk
  • wateja wako wataweza kutoa feedback za huduma zako ambazo zinaweza kusaidia kuvutia wateja wengine.
  • na nyingine nyingi

Zifuatazo ni hatua za kufata ili kufanya taarifa za bishara yako zionekane kwenye google map.

  • Hakikisha una application ya google map kwenye simu yako. Kwa watu wanaotumia Android inakuepo moja kwa moja na kwa watumiaji wa iPhone (iOS) unaweza download kutoka app store. Icon yake ni kama hii picha
Icon ya google map
  • hakikisha umewasha location yako (Switch location on)
  • Ingia kwenye app ya google map
  • Upande wa kushoto juu kabsa bonyeza icon inaonekana kama mistari mitatu.
  • Shuka chini hadi utakapoona neno “add a missing place”. Bonyeza hilo neno
  • Itafunguka page mpya ambayo ndio utajaza taarifa za biashara yako kama ifuatavyo.

NAME: — andika jina la biashara yako

ADDRESS: — bonyeza "Mark location on map". kama umewasha location na upo sehem ya duka lako, basi alama ya location itaonekana sehem ulipo moja kwa moja. Kama haupo sehem ya duka lako wakati huo basi itafte kwenye ramani

CATEGORY: — Hapa utachagua category ya biashara yako. unaweza tafta kwa kusearch ama kwenye list.

bonyeza add phone, hours na photo kuongeza taarifa zaidi za biashara yako

HOURS:- Bonyeza "days and hours", itafungua page mpya ambayo unaweza kuongeza siku na mda ambao duka lako lipo wazi. kwenye page ya "add hours" bonyeza "select days hours", hapo utaanza kwa kuchagua siku ambazo duka lako lipo kisha bonyeza "next" kuchagua mda ambao dula lipo wazi.

PHONE:- Weka namba ya simu unayotumia

WEBSITE:- weka jina la website yako. Kama hauna unaweza kuweka hata link yako ya instagram, Mfano kama instagram usernama yako ni "atistore_tz' basi unaweza andika "https://www.instagram.com/atistore_tz". Pia sio lazima kuweka website kama hautaji au hauna.

OPENING DATE:- Hapa unataweka siku ambayo ulifungua duka lako

PHOTO:- Weka picha za biashara na duka lako.

Baada ya kumaliza hatua zote hizo utabonyeza icon upande wa juu kulia. Fuata hatu zote zinazofuata ni rahisi na zipo moja kwa moja.

Itachukua mda kidogo hadi taarifa zako ziweze kutokea Google. Mara nyingi ni chini ya nusu saa.

Kama umefanikiwa kila kitu basi ukisearch jina lako kwenye google itaonekana kama mfano wa picha hapa chini.

Karibu sana.

Personal contacts

Instagram: @saadjumbe | WhatsApp/Call/Text: 0786503601

Company contacts

www.pralena.com

--

--

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI

Serial entrepreneur with a passion for any kind of tech that can push human progress forward. Much involved in #FinTech #DigitalMarketing #UI/UX.