TP 1: JE AKAUNTI YAKO YA INSTAGRAM NI BUSINESS ACCOUNT ? HIZI NI FAIDA ZAKE

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI
3 min readAug 12, 2018

Instagram ina aina kuu mbili za akaunti:-

  1. Akaunti ya kawaida (personal account)
  2. Akaunti ya biashara (business account).
Kushoto ni akaunti ya biashara na kulia ni akaunti ya kawaida

Baadhi ya faida za kua na akaunti ya biashara kwa mfanyabiashara ni:-

  1. uwezo wa kujua ni mda gani upost bidhaa yako ili kufikia watu wengi zaidi.
  2. Ni aina gani ya bidhaa/huduma hupendelewa na followers wako,
  3. Idadi ya watu wapya wanaotembelea akaunti yako kila siku kwenye account yako,
  4. followers wapya wanatokea mkoa ama nchi gani n.k

kama mfanyabiashara business account inakupa faida nyingi sana kama zilivyoaanishwa hapo juu, faida kuu ikiwa kuweza kufanya matangazo (sponsored ads) na pili kupata insight(taarifa) za followers na post zako.

SPONSORED ADS: haya ni matangazo ambayo hufikia mtu yeyote hata kama hajafollow account yako. Instagram hukusanya data(taarifa) nyingi za watumiaji wake ambazo hutumika kumsaidia mfanyabiashara kufikia watu wenye uhitaji wa bidhaa yake kwa njia ya matangazo. Baadhi ya taarifa hizo zinazokusanywa ni umri, jinsia, mahali unapoishi na bidhaa unapendelea kuangalia kwenye mtandao.

INSIGHT: hizi ni data(taarifa) zinazokusaidia kutambua zaidi followers wako na watu wanao pitia account yako. kupitia insight utafahamu asilimia kubwa ya followers wako wanatokea wapi, umri wao n.k. Pia unaweza kufahamu ni aina gani ya post ambazo zinafikia watu wengi zaidi. Insight inakusaidia kujua ni sehem/namna gani uboreshe biashara yako.

FIG: KUSHOTO NI AKAUNTI YA BAISHARA NA KULIA NI ACCOUNT YA KAWAIDIA

FUATA HATUA HIZI KUBADILI AKAUNTI YAKO KUA YA BIASHARA

Tufollow kwenye mitandao ya kijamii

instagram & Twitter: Saad Jumbe

au

Instagram & twitter: Pralena Network Limited

--

--

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI

Serial entrepreneur with a passion for any kind of tech that can push human progress forward. Much involved in #FinTech #DigitalMarketing #UI/UX.