URAHISI WA KUUZA NA KUNUNUA BIDHAA INSTAGRAM KWA KUTUMIA HASHTAG (#BIDHAATZ)

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI
3 min readApr 15, 2018

Instagram ni moja ya mtandao wa kijamii wenye watumiji hai (active member) wengi nchini Tanzania. Matumizi ya mtandao huu yamejipanua sio tu baina ya mtu na mtu bali hata kua fursa kwa wafanyabiashara kufikia wateja wao.

Kuna zaidi ya wafanyabishara 3000 nchini Tanzania wanaotumia Instagram kama njia mbadala ya kuuza bidhaa zao. Mtandao unamsaidia mfanyabishara kukuza wigo wa soko, kwa kutotegemea wapita njia tu. Mtandao unampa uwezo mfanyabishara aliepo Mbagala, Dar es salaam kumfikia mteja aliepo Kashai, Bukoba.

CHANGAMOTO

Kama ilivyo kizuri hakikosi mapungufu. Changamoto zilizopo Instagram ni ugumu wa kutafta(search) bidhaa unayoitaka na kuipata moja kwa moja kama ilivyo kwenye Facebook na Google.

mfano tafta(search) neno sneakers kwenye Facebook, Google na Instagram.

GOOGLE:

matokeo itakua links za tovuti (website) au picha za sneakers kutoka katika tovuti mbalimbali. UTAONA BIDHAA MOJA KWA MOJA

FACEBOOK:

Hapa itaonesha machapisho (post) zote zenye neno “sneakers” kutoka katika groups, video, page nk. UTAONA BIDHAA MOJA KWA MOJA

INSTAGRAM:

Matokeo ni hashtag na akaunti(account) zinazotumia neno sneakers na sio post za bidhaa moja kwa moja. Utatakiwa kuchagua hashtag au account.

maelezo maelezo kwa picha

Hii ni changamoto ambayo inakosecha wafanyabiashara kujipatia wateja wengi zaidi na wateja kujipatia bidhaa wanazotaka kirahisi.

MAPENDEKEZO

Kwa ushilikioano baina ya BongoAds na wafanyabiashara mambo mawili yalipendekezwa

  1. Kutoa elimu ya matumizi ya sahihi ya hashtag kwa wafanyabishara na wateja wao
  2. Kuchagua mtindo wa hashtag zenye ufanano ili kuleta urahisi wa kutafta bidhaa tunazotaka kutoka Tanzania.

Hashtag mama itakua inatumika ni #bidhaatz, utaona bidhaa zote za wafanya biashara kutoka Tanzania .

Na pia kama utataka bidhaa flani utaadika jina lake kisha utamalizia neno tz mfano unataka #snickers basi utaandika #sneakerstz. Hapo utaona bidhaa za wafanyabishara wanaouza sneakers kutoka Tanzania .

UMUHIMU WA KUTUMIA HASHTAG #BIDHAATZ NA #TZ

Matokeo baada ya kutafta sneakers na sneakerstz

Mapendekezo ya kutumia hashtag zenye neno “tz” kuleta urahisi wa kupata bidhaa za wafanyabiashara wa Tanzania.

Mfano ukitafta neno sneakers matokeo yatakua million 22. Hashtag hii inatumika Duniani kote hivyo sio rahisi kujua hii bidhaa inauzwa na mtanzania ama la.

Pia ukitafta neno sneakerstz matokeo yatakua machache sana. Umuhimu wa kuweka neno TZ ni kuleta rahisi wa kupata bidhaa za Tanzania kama ilivyo kwenye picha hapo juu.

CONCLUSION

KWA MFANYABISHARA

hakikisha unatumia hashtag wakati una post bidhaa zako.

  1. Weka #bidhaatz kama hashtag mama
  2. Andika jina la bidhaa unayouza mfano #sneakerstz, #jordantz etc
  3. Ongeza hashtag za majia ya jumla ya bidhaa mfano #viatutz, #kiatutz #shoestz n.k

MTEJA

Ni rahisi ingia instagram search jina la bidhaa unayotaka mfano #vyombotz kisha bonyeza hashtah kuona bidhaa zote za vyombo kutoka kwa wafanyabishara wa Tanzania.

kwa maelezo zaidi follow akaunti zetu instagram

Bongods
Ammashops
Saad jumbe

--

--

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI

Serial entrepreneur with a passion for any kind of tech that can push human progress forward. Much involved in #FinTech #DigitalMarketing #UI/UX.