CLICK TO CHAT

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI
1 min readNov 2, 2018

Hii ni huduma ya whatsapp inayoondoa usumbufu wa ulazima wa kusave namba ya mtu kwanza ndio uweze kuchat nae.

huduma hii inaweza kutusaidia pale tunapofanya matangazo ya sponsored au kuweka link kwenye bio instagram (ama mtandao mwingine) ikiwa tuanataka mtu awasiliane na sisi moja kwa moja WhatsApp.

Link inakua kama hii

https://api.whatsapp.com/send?phone=255786503601

ukibonyeza (click) tu hyo link itafungua chat moja kwa moja na mtu ataweza kuchat na wewe bila ya ulazima wa kuanza kusave namba kwenye simu yake.

NAMNA YA KUTENGENEZA LINK YAKO

https://api.whatsapp.com/send?phone=

Copy hiyo link hapo juu na kisha baada ya alama ya Sawasawa(=) unganisha namba yako ya simu ukianza na country code (usiweke alama ya kujumlisha).

Mfano namba yangu ya whatsapp ni 0786503601 na Country code ya Tanzania ni +255. Hivyo ambayo nitayounganisha na link itakua 255786503601

link iliyokamili itakua hivi

https://api.whatsapp.com/send?phone=255786503601

KUMBUKA

  1. Namba yako ianze na country code (usiweke alama ya kujumlisha) mfano Tanzania ni 255 . iwe mfumo wa hivi 255786503601
  2. Hakikisha hauachi nafasi kati ya herufi/namba
  3. kumbuka kila nchi ina country code yake (Tanzania ni +255)
  4. Hakikisha namba yako inatumika whatsapp

Personal contacts

:Instagram: @saadjumbe | email: saadjumbe@gmail.com

Company contacts

instagram: @pralenanetwork |email: info@pralena.com |www.pralena.com

--

--

Saad Jumbe
KUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI

Serial entrepreneur with a passion for any kind of tech that can push human progress forward. Much involved in #FinTech #DigitalMarketing #UI/UX.