Kuwa Wewe Bila Samahani

Sandrahope Msigwa
Love Shack
Published in
2 min readSep 20, 2023

Haudaiwi ufafanuzi wowote juu ya kuwa wewe.

“Mkubwa au mdogo unakila kitu ili kuwa wewe. Kuwa wewe kutakufanya upate kipaumbele na sifa njema ambao wengi wanatamani kupata. Kuwa na ujasiri wa kuonyesha watu wengine jinsi wewe ulivyo tofauti ndicho kinacholeta heshima, sio kufanya ambavyo wengine wanafanya kwasababu unaogopa hawatakukubali jinsi ulivyo” — Rob Hausler.

Kila mtu kwenye hii dunia ana dhumuni la kutimiza na ili wewe utimize dhumuni ulilopewa na Mungu kwenye maisha yako inabidi ufwate njia yako na kuwaachia wengine wafwate njia yao katika safari ya maisha.

John Mason alishawahi kusema “Huwezi kufika hatima yako kwa kutumia barabara ya mwengine. Unapotembea njia yenye alama ya walipopita wengine huwezi kuvumbua kipya.” Na pia “Unapo jaribu kuwa kama mtu mwengine, utakuwa wa pili bora”.

Jiweke huru na viwango vya mitandao ya kijamii na viwango vya wengine kisha jiwekee mwenyewe viwango vyako ili uweze kuwa toleo bora la kwako mwenyewe.

Ni Muhimu Kuwa Wewe Kwasababu:

  1. Unakuwa mwenye furaha unapokuwa wewe.
  2. Utaweza kuzingatia mwelekeo wako na utajua jinsi ya kuongoza maisha yako.
  3. Itakuwa rahisi kujenga utambulisho wako kwa kutambua maadili na imani yako.
  4. Unakuwa jasiri juu ya maamuzi yako; kujijua kunaruhusu wewe kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yako na kupata ujasiri ya yajayo kutokana na maamuzi hayo.
  5. Unapata marafiki wa kweli na wakubaki nao; ukiwa wewe unavuta na kupata watu ambao mna maslahi ya kuendana na hautahitaji kuwa feki ili kukaa nao.

Usiruhusu watu wengine kukubadilisha. Utahukumiwa tu haijalishi ufanyaje.

Kabla ya kujibadilisha au kubadilisha kitu kwenye maisha yako jiulize unajibadilisha kwasababu mtu kakusema vibaya? au unajaribu kumfurahisha mtu? unajaribu kufaa na watu fulani?. Kama jibu ni hapana kwa maswali yote haya basi vyema endelea. Kama jibu ni “Ndio” naomba ujue hatuwezi kubadilisha jinsi watu wanatufikiria/kutusema/kutufanyia na zaidi hatuwezi kuachia maneno au maamuzi yao kuendesha maisha na tabia yetu.

“Thamani yako haishuki kisa mtu mwengine ameshidwa kuiona”

Kwa Upendo,

Sandrahope M.

--

--