Siri Ya Upendo Unao Dumu

Sandrahope Msigwa
Love Shack
Published in
4 min readFeb 13, 2022

Ni jinsi unavyoyaonyesha!

Upendo ni kama lugha yoyote nyingine. Kadri unavyo jifunza, inazidi kuwa rahisi.

Na kama lugha nyingine kuiongea na kuielewa ni tofauti na ngumu ni kama kichina na kiswahili haijalishi unaongeza sauti kiasi gani haita mfanya mchicha aelewe kiswahili.

Kwenye upendo kuonyesha na kuhisi ni tofauti pia, haijalishi nguvu kiasi gani kuonyesha unampenda mwenza wako kama unaonyesha kwa lugha ya upendo ambayo sio yao basi hawato kuja kuhisi wanapendwa kwasababu kinachofanya wewe uhisi unapendwa haimaanishi yeye itamuonyesha anapendwa.

Ni nadra sana kuwa wenza wawili wanakuwa na lugha moja ya upendo. Kila mmoja wetu ana lugha ya kuzaliwa na ndio lugha tunajua kuiongea zaidi kwahiyo kila mtu ana lugha yake msingi ya upendo. Na kwa asili huwa tunaongea lugha yetu sisi lakini tunaweza kujifunza lugha nyingine.

Lugha 5 za Upendo — Gary Chapman

❤️ Maneno ya Kuthibitisha: Kwa watu hawa maneno ya kuhamasisha, kutia moyo, kuthamini, shukrani huwa yana maana zaidi kwao. Kuongea lugha hii tafuta vitu vyao vizuri na onyesha upendo kwa kuwaambia uzuri wao.

🚫 Kwa watu wenye lugha hii ya upendo epuka kukosoa bila kujenga na kutokutambua au kuthamini juhudi zao kwa kuwa haya yanawaumiza sana.

❤️ Muda Bora: Kumpa mwenza wako umakini usiogawanyika kwa mfano kukaa sehemu tv ikiwa imezimwa, kuto kutumia simu au kutembea wote sio kwa ajili ya mazoezi ila tu kuwa wote. Muda Bora haimanishi kwenda mgahawani na kila mmoja yupo anashughulika na simu yake maana hapo mtakuwa mmefuata chakula tu.

🚫 Kwa watu wenye lugha hii ya upendo epuka usumbufu au shughuli nyingine ukiwa nao, na pia epuka kukaa muda mrefu bila kuwa na muda wa pamoja na hata kutumia muda mwingi na marafiki kuliko mwenza wako.

❤️ Matendo ya huduma: Kwa watu hawa matendo yana nguvu zaidi ya meno na kuongea lugha hii unahitaji kujua ambacho wao wanapenda uwafanyie mara kwa mara. Hii inaweza kufanya kazi za nyumbani, kuwasaidia kufanya kazi tofauti ata kubadilisha nepi ya mtoto.

🚫 Kwa watu wenye lugha hii ya upendo epuka kuweka maombi ya wengine kipaumbele au kupotezea maombi yao na hata kufuatalia maswala madogo madogo au makubwa.

❤️ Kupokea zawadi: Kwa wengine wanapo pokea zawadi inaonyesha huyu mtu alikuwa ananifikiria. Kujua aina ya zawadi kuwapa uliza maswali na chunguza. Kujitoa kwako pia wakati mwenza wako anakuhitaji kama kwenda nae hospitali pia inaongea zaidi kwa watu waopenda kupokea zawadi kwakuwa unakuwa umetoa zawadi ya uwepo wako.

🚫 Kwa watu wenye lugha hii ya upendo epuka kusahau sikukuu muhimu au kuwapa zawadi bila kuwa na shauku kwa kuwa ata jinsi unavyowapa zawadi ina maana zaidi kwao.

❤️ Mguso wa mwili: Kwa watu hawa mguso sahihi inaongea kupendwa sana kwao. Mguso sahihi ni upendo na mguso usiofaa ni isiyo na heshima. Kumbuka kila tamaduni ina miguso sahihi na isiyofaa kwa watu wa jinsia tofauti. Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanaoshikwa na kukumbatiwa huwa wanakuwa na hisia busara kuliko ambao wanapita muda mrefu bila kushikwa.

🚫 Kwa watu wenye lugha hii ya upendo epuka kupuuza mahitaji yao ya kimwili au kukaa muda mrefu bila kuwapa ukaribu wa kimwili na muhimu zaidi usiwa nyanyase kimwili (hii inaenda kwa kila mtu pia).

Jinsi ya kujua lugha yako ya upendo: 1. Chunguza jinsi unavyo onyesha upendo kwasababu mara nyingi hiyo inakuwa ndo lugha unayotamani kupata. 2. Andika malalamiko na maombi yako kwasababuu hapo ndipo hitaji lako lilipo. 3. Jaribu kuchukua jaribio kwenye tovuti www.5lovelanguages.com.

Dhana potofu iliyopo hasa katika ndoa na familia za ki Afrika ni kwamba wanaume wanaelewa upendo kwa “matendo ya huduma” (kupika, kusafisha nyumba n.k) na wanawake kwa kupokea zawadi (vitu vitu). Na watoto wanakuwa wakiona wazazi wao wanachofanyiana kama upendo na wao wanaenda tena kuweka kwenye ndoa zao bila kujifunza hitaji la mapenzi la mwenza wao.

Usikisie, Chagua kujifunza lugha ya mwenza wako

Binadamu wote tuna hitaji la kupendwa. Hii inamaanisha tuna tenki la hisia ya upendo na mapenzi yakionyeshwa kwa njia sahihi inajaza tenki hilo. Huwa tuna kuwa tofauti wakati tenki la hisia la upendo likiwa limejaa au likiwa tupu. Mahusiano yakiwa na mmoja au wote matenki ya hisia ya upendo ikiwa tupu ni kama kuenedesha gari bila mafuta hata kuendesha gari ikiwa ina mafuta machache kila siku inaharibu gari, unaishia kuharibu gari na upendo usipokuwa unaonyeshwa kwa lugha husika unaharibu mahusiano yako.

💡Noti : Lugha hizi za mapenzi zinatumika kwa watoto adi vichanga pia, kwa watoto utahitajika kuongea lugha zote adi utakapojua mwanao anaelewa lugha gani zaidi na uionyeshe ili tenki lake la hisia ya upendo lijae.

Dr Gary Chapmana anasema pia “ Ndani ya kila mtoto kuna ‘tenki la hisia ya upendo’ likisubiri kujazwa na upendo. Mtoto akihisi anapendwa, ata kuwa kwa kawaida ila tenki la hisia ya upendo likiwa tupu mtoto anakuwa mtukutu. Utukutu wa mtoto huwa unahamasihwa kwa mahitaji ya tenki la hisia ya upendo lililo tupu.”

Uonyesha lugha hizi 5 za upendo kwa watu wote na yeyote. Mwenza wako,watoto, wazazi, wakwe, marafiki, ndugu, wageni na hata kwako. Onyesha upendo kwakuwa wote tunahitaji.

“Sasa yanadumu haya matatu: Imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.”- ‭‭1 Wakorintho‬ ‭13:13‬ ‭BHN‬‬

Kwa Upendo,

Sandrahope M.

Rejea:

The 5 Love Languages: The Secret to Love That Lasts by Gary Chapman.

--

--