Mimi ni Mchimbaji Nahitaji kuanzisha maabara ya kupima madini. Naanzaje?

Johansen
4 min readFeb 5, 2024

--

Nimekuwa mikikutana na maswali mengi kama haya kutoka kwa wachimbaji wa madini hasa wa dhahabu, wakitamani kuanzisha maabara za kupima sempo kama biashara au sampuli za wateja wao.
Nimekuwekea mambo muhimu ya kuzigatia kabla hujaanzisha maabara sehemu yoyote

Nikupe historia kidogo ya maabara za madini

Hii ni teknolojia iliyoanzishwa na wazungu kwa ajili ya kusaidia katika shuguli zao za uchimbaji
Kabla haijafika tanzania imeanzia nchi kama south afrika na zimbabwe ambazo zilikuwa na kiwango kikubwa cha dhahabu.

Tanzania hii teknolojia imeanza baada ya kuanzishwa kwa migodi mikubwa kama GGM na Buzwagi, hao wachimbaji wakubwa walikuja na makampuni kama SGS kwa ajili ya kuwasaidia kupima kazi zao za uchimbaji

Walipokuja hao wazungu wakasababisha uhitaji wa wataalamu ukawa mkubwa sana ndipo zikaanzishwa kozi mbalimbali za madini katika chuo cha dar es salaam.

Hizo maabara za wazungu zikachukua watanzania wakaenda kusoma nje ya nchi, waliporudi wakawa wanafanya kazi kwenye hizo maabara na baadhi wakaanzisha maabara zao binafsi kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Kuanzisha maabaya ya kufanya vipimo

Kuanzisha maabara ya kupima madini ni mradi wa kawaida sana kwasababu hauna mambo mngi sana, kikubwa unahitaji uwe na mipango na malengo sahihi.

Hapa kuna vitu muhimu vya kuzingatia kabla ya kuanza biashara ya maabara ya kupima madini:

Kwanza kuna maabara za aina mbili

  1. Maabara ya biashara
  2. Maabara ya kufanya kazi zako binafsi

Maabara ya biashara inakuwa kama kiwanda maana inafanya kazi nyingi sana
maabara ya binafsi inakuwa inapima kazi zako tu au za mgodi wako tu

Kumbuka: Pesa utakayoitumia kupima sampuli zako kwenye maisha yako ya uchimbaji ni nyingi sana ukilinganisha na utakayotumia ukiwa na maabara yako mwenyewe

1. Fanya Utafiti wa Soko na Upatikanaji wa Wateja

Fanya utafiti wa kina kuhusu soko la upatikanaji wa wachimbaji na mahitaji ya wachimbaji wa eneo lako.
Tathmini ni aina gani ya huduma za upimaji wa madini wanazohitaji na angalia ushindani uliopo

Maabara za madini ni kama hospitali, ukimpimia mchimbaji kazi yake vizuri, lazima tu atarudi kwako. na siku zote wachimbaji wanatafuta maabara itakayowapimia vizuri wakapata faida

2. Sheria na Kanuni za eneo

Hakikisha kuwa unafahamu na kuzingatia sheria na kanuni zote zinazohusiana na biashara ya madini katika eneo lako.
Pata leseni zote muhimu na kufuata taratibu zinazohitajika.

Kama ni nje ya Tanzania, Uganda, Kenya, Kongo, Burundi
Hakikisha unafata sheria zote
Huwezi kufanya maabara kimyakimya, kwasababu jina lake linakua kwa sana, ni vyema ukafata sheria zote na sheria za mazingira ili kuepuka usumbufu

Nimefanya kazi za maabara Tanzania, Kenya naUganda. Kila nchi ina taratibu zake na sera zake za kuishi na watu

3. Miundombinu na Vifaa

Kuna makala hii niliandika kuelezea miundimbinu na vifaa vya maabara, unaweza kuipitia https://medium.com/@johansentz/jinsi-maabara-za-kupima-madini-zinavyowatajilisha-wachimbaji-wa-dhahabu-tanzania-d944607e1b71

Weka au andaa miundombinu inayofaa kwa ajili ya maabara, ikiwa ni pamoja na nafasi ya kutosha, vifaa vya usalama, na mahali pa kuhifadhi sampuli.

Unaweza kujenga jengo lako au ukapangisha jengo
Vifaa vinapatikana china , australia, south africa au hapa Tanzania vinapatikana unaweza kunitafuta whatsap nikakusaidia Bonyeza hapa https://wa.me/qr/FIZNXJYNQYULE1 au namba hii +255757915043

4. Wataalamu na Wafanyakazi

Tumia wataalamu wenye uzoefu katika maabara za madini. Ukiwa na wataalamu wazuri utafanya kazi nzuri, utatengeneza jina kubwa sana na wateja watakuwa wengi sana.
Wataalamu wapo wengi sana wenye uzoefu

5. Usalama wa Mazingira na Afya

Jitahidi Maabara iwe mbali na makazi ya watu, iwe na barabara nzuri, unaweza kumwelekeza mtu akafika kwa wakati.

watu wa mazingira watakuja kukagua

6. Matangazo na Masoko

Hii sio muhimu sana lakini inasaidia sana unapoanza, anapokuja mchimbaji mmoja, anawaleta wenzake kumi
KIkubwa ni kutoa huduma bora na ya uhakika wateja watakuja wengi sana

Kama maabara yako ni ya kazi zako binafsi, kuwa na mtaalamu mmoja au wawili ambao watafanya kazi zako na kutunza vifaa vyako

Kwa ushauri zaidi nipigie whatsapp namba

https://wa.me/+255757915043

Tumia hizi mbinu ili maabara yako ipate wateja wengi

Baada ya kufungua maabara, unahitaji kufanya hivi ili kuvutia wateja wengi sana +255757915043

  1. Tengeneza mfumo ambao

Itaendelea

--

--

Johansen

blockchain and Cryptocurrency researcher and content writer